CCM NJOMBE WATOA KAULI KUFUTWA ADA KIDATO CHA V-VI

0

MAPENDEKEZO ya kufutwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita yaliyosomwa kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2022/23, yamepongezwa na Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Njombe.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa Njombe, Scholastika Kevela, umetoa pongezi hizo leo, siku moja mara baada ya kusomwa mependekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2022-2023, ambayo pamoja mambo na mengine imependekeza kufutwa kwa ada hiyo, kwa wanafunzi wa vidato hivyo.

Hatua hiyo ni muendelezo wa mambo mbalimbali makubwa yanayoendelea kufanywa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, tangu aapishwe mwaka mmoja uliopita.

" UWT Mkoa wa Njombe tunazidi na tutazidi kuendelea kumpongeza Rais Samia kwa hatua nyingi anazozifanya kuwapunguzia mzigo Watanzania , amefuta vilio vya masikini wengi waliokuwa wakihaha kutafuta hela kuwalipia watoto wao ada," alisema Kevela.

Akisoma mapendekezo ya bajeti ya serikali jana bungeni, Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, alisema katika utekelezaji wa bajeti hiyo, Rais Samia alitoa mapendekezo ya kuondolewa kwa ada hiyo hatua ambayo kila Mtanzania ameipokea kwa furaha.

"Watanzania watake nini zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Njombe nikiwa Mwenyekiti wao UWT niwatake wanawake wenzangu waliopo kila kona ya Tanzania kujitokeza na kuzitangaza kazi nzuri anazozifanya Rais Samia," alisisitiza  Scholastika Kevela.

JE! UMESIKILIZA WIMBO HUU,KAMA HUJASIKILIZA USIPITWE BOFYA KUSIKILIZA 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top