Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh. Juma Sweda ameagiza gari la Kituo cha Afya Ikuwo lirudishwe Kituoni hapo mapema iwezekanavyo kwa lengo la kutoa huduma kwa wagonjwa.
Ametoa agizo hilo kwa Mganga Mkuu Wilaya ya Makete baada ya kufika Kata ya Ikuwo na kukutana na malalamiko ya wananchi wa Tarafa ya Ikuwo ambao wamesema wanapata changamoto kubwa ya usafiri wakati wanapopata dharura ya wagonjwa
Imeelezwa kuwa gari hiyo ipo kwenye Matengenezo Wiwlayani kwa muda sasa na inakaribia kukamilika
Wananchi wa Kata ya Ikuwo na Kigala wamekuwa wakitegemea gari hilo kupata huduma ya kusafirisha wagonjwa kwa gharama ndogo kwa kusafirisha wagonjwa kupeleka Hospitali ya Wilaya, ambapo kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu wamekosa huduma hiyo
Baada ya wananchi wa Tarafa ya Ikuwo kuwasilisha changamoto ya Barabara ya Usalimwani, Ikuwo-Nkenja kwa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhandishi kutoka TARURA Ndg. John Kawogo amesema serikali imetenga fedha Milioni 140 kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Usalimwani, Ikuwo mpaka Nkenja
Mhandisi Kawogo amesema tayari Ujenzi wa Barabara kutoka Usalimwani mpaka Ikuwo unaendelea na wanategemea kuanzia mwezi wa nane 2022 wanatarajia kuanza Matengenezo kutoka Matenga kuelekea Nkenja.