Wakazi wa kijiji cha Mahongole kilichopo halmashauri ya Mji wa Makambako wilayani Njombe Wameitaka serikali kuwasaidia kupata ardhi yao yenye ukubwa wa ekari 1001 iliyochukuliwa na muwekezaji wa kigeni kutoka Kampuni ya DL Group ama kulipwa fidia ya kupisha maeneo hayo ambayo waliayatoa baada ya muwekezaji huyo kukiahidi kijiji kujenga Bandari Kavu na viwanda vya kuzalisha nguo,chuma na parachichi.
Wakazi hawa wanasema 2019 muwekezaji huyo kutoka Kenya alifika kijijini kwao kuomba ardhi ya kuwekeza viwanda na kisha kuahidi kulipa fidia lakini hadi sasa inaelezwa ni ekari 371 tu zilizolipwa fidia jambo ambalo limezidi kuongeza umasikini kwa familia zizilizopisha mradi huo kwa miaka mingi bila kufanya uzalishaji.
Kufuatia changamoto hiyo waliyokiri kuwarudisha nyuma kimaeneleo Wakazi hawa akiwemo Chesko Sambala wanatumia mkutano wa hadhara uliyoitishwa na mkuu wa wilaya ya Njombe wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi kuomba serikali kuwasaidia kupata maeneo yao ama fidia ya fedha kwasababu tangu muwekezaji achukua ardhi hiyo miaka mine iliyopita ametoweka na hakuna ujenzi wa viwanda na bandali kavu unaofanyika kama walivyoelezwa.
Mara baada ya kusikia kero hiyo na ukubwa wa eneo lililochukuliwa kwa zaidi ya miaka 4 bila kuendeleza ndipo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa akaomba kupewa wiki mbili kulifatilia sakata hilo huku diwani wa kata ya Mahongole Mario Kihombo uharaka unatakiwa kutatua mzozo huo.
TAZAMA WANANCHI WAKITOA KILIO CHAO KWA MKUU WA WILAYA,NAYE AOMBA MUDA KUJIBU KERO ZA WANANCHI HAO.