Ni kweli kuwa biashara nyingi siku hizi zina hamia mtandaoni, hii ni kutokana na urahisi wa mawasiliano unaoletwa na teknolojia. Lakini ni wazi kuwa kama binadamu sio kila mara unaweza kuwa na simu yako mkononi ukiwa tayari kuchat na wateja.
Kuliona hili nimekuletea apps nzuri ambazo zinaweza kukusaidia sana kujibu meseji za WhatsApp za wateja wako bila wewe kufungua simu yako au kujibu meseji hizo wewe binafsi.
Kupitia makala hii utaweza kupata kujifunza jinsi ya kutumia APP ya Skedit kutuma SMS Bila kushika simu yako! hatua kwa hatua.
SKEDit Scheduling
SKEDit ni app nzuri sana ya Android ambayo inakusaidia kufanya meseji za WhatsApp zijitume zenyewe, mbali ya WhatsApp app hii inaweza kufanya mambo mengi sana kama vile kusaidia status kwenye mtandao wa Facebook zijiposti zenyewe, kusaidia barua pepe ijitume yenyewe pamoja na meseji za kawaida SMS nazo unaweza kufanya zijitume zenyewe kupitia App hii,lakini pia inaweza kukukumbusha kupiga simu unapokuwa umetingwa na kazi.
TAZAMA VIDEO JINSI YA KUTUMIA APP HII ITAKUSAIDIA BURE KABISA