Kiongozi wa Mwenge agoma kukabidhi Pikipiki kwa Vijana walioshindwa kutafsiri Alama za Barabarani

0

 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa Mwaka 2022 Sahil Geraruma amegoma kukabidhi Pikipiki kwa baadhi ya vikundi vya Madereva wa bodaboda ambao wamenufaika na mkopo wa asilimia kumi kutoka Halmashauri kutoka na baadhi yao kushindwa kutafsiri Sheria na alama za Barabarani.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Babati Mkoani Manyara kwaajili ya kukagua miradi mbalimbali.
Kiongozi huyo wa Mwenge Gereruma amesema lengo la Serikali nikuhakikisha asilimia kumi ya mpango wa kila Halmashauri unawafikia walengwa ambao ni Vijana, kina mama pamoja na watu wenye Ulemavu lakini hawezi kuruhusu vijana kuingia barabarani wakiwa hawafahamu alama za barabarani.
“Mimi siwezi nikaondoka alafu nikasikia Kuna mtu kaangia kwenye uvungu wa fuso kakatwa miguu,sitaki kusikia kitu kama hicho Sasa nataka kuacha madereva ambao wanajielewa”- Geraruma

Amegiza Pikipiki hizo kurudishwa katika ofisi ya Mkurugenzi na kukabidhi leseni hizo kwa Kamanda wa Polisi Wilaya na kuagiza vijana hao kupatiwa Mafunzo ya Wiki moja ili kufahamu na kujua Sheria na Alama za barabarani.
Mwenge wa Uhuru upo Wilaya Babati ukitokea Wilaya ya Kiteto ambapo utakimbizwa katika Wilaya zote zilizopo Mkoa wa Manyara, Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 zitafikia kilele chake Oktoba 14, 2022 mkoani Kagera zenye kauli mbiu Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo Shiriki kuhesabiwa, tuyafikie Maendeleo ya Taifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top