KUPANDA KWA MBOLEA KERO KWA WANUFAIKA WA ASILIMIA 10% ZA HALMASHAURI

0

Wakati baadhi ya vikundi vya wakulima wakipatiwa mkopo wa asilimia 10% toka Halmashauri ya mji wa Njombe kwa ajili ya kuendeleza shughuli za maendeleo,Kikundi Cha Amani  kilichopo Iwungilo kilichopatiwa Milioni tano kwa ajili ya Kilimo Cha Viazi mviringo  kimesema Kupanda mara dufu kwa mbolea kumekuwa kikwazo kikubwa kwao.

Katika ziara ya kikazi ya mkuu wa wilaya ya Njombe katika kata ya Iwungilo Kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo Kikundi hicho Cha Wanawake watano waliopata Fedha hizo wamezielekeza shambani ambako wanatarajia kuvuna katika siku za usoni Wamesema pembejeo za Kilimo zimekuwa Changamoto kubwa.

Apronia Lwiva na Benadetha Chaula ni wanakikundi cha Amani ambao wanalia na gharama kubwa za pembejeo licha ya kuwa na Malengo makubwa

Afisa Kilimo Halmashauri ya mji wa Njombe Ernest Ngaponda amesema katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha Ujao serikali itaweka Ruzuku kwenye Mbolea Ili kuwanusuru wakulima na Gharama hizo.

Godfrey Mhando ni Diwani wa kata ya Iwungilo ambaye anakiri kushuhudia ujenzi wa kiwanda kikubwa Cha Mbolea huko Dodoma ambapo anaamini kitakuwa muarobaini wa Changamoto ya mbolea huku mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa akieleza sababu za kupanda kwa bei hiyo.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Njombe Enembola Lema Amesema Zaidi ya Milioni 100 za mikopo zimetolewa kwa vikundi vya kata ya Iwungilo Hadi sasa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top