Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu amesema kuwa ipo haja ya kuwaandaa vijana wa kiume ili kuja kuwa baba bora wa familia kama wanavyoandaliwa mabinti ili kupunguza matukio ya mauaji, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vilivyoshamiri hivi sasa nchini.
Akihojiwa na moja ya chombo cha habari nchini, Msambatavangu amesema; "Juzi niliongea jinsi mtoto wa kiume anavyolelewa hatumwandai kuwa baba wa familia. Tunajikita sana kuwaandaa watoto wa kike na tunawasahau watoto wa kiume.
"Hata kwenye harusi kitchen Party na Sendoff tunawafanyia watoto wa kike na hawa kiume inakuwaje? Nashauri watoto wa kiume wafanyiwe Sendoff au bagparty," amesema Msambatavangu.