MGAMBO WADAIWA KUJERUHI WAWILI WAKIONDOA MACHINGA GEITA MJINI

0

Askari Mgambo wa Halmashauri ya mji wa Geita waliokuwa wakiondoa  Wamachinga maeneo yasiyo rasmi katika Mtaa wa shilabela Geita Mjini  wanadaiwa kupiga wamachinga hao na kujeruhi watu wawili.

Waliojeruhiwa ni pamoja na Laizer Peter (14 ) Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza  Shule ya Sekondari Nyanza  mjini Geita anadaiwa kupigwa na nondo kichwani na askari mgambo  na kudaiwa kusababisha kipande cha chuma kuingia kunasa kichwani.

Mama mzazi wa kijana huyo Siwema Jacob amesema kuwa mtoto alimuagiza dukani kununua dawa na Baada alirudi akiwa anavuja damu kutoka kichwani akieleza kuwa amekutana na Mgambo wakampiga .

Mama anasema kuwa mtoto wake alipelekwa kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa Geita lakini Baada ya uchunguzi wa X-ray ilibainika kibande cha chuma kimechoma hadi Kwenye fuvu la kichwa hivyo akapewa rufaa kwenda Bugando .

Ameeleza kuwa Laizer ameisha fanyiwa upasuaji na anaendelea na matibabu lakini Hali yake siyo nzuri.

Mtu mwingine aliyejeruhiwa ni  kijana aliyejulikana Kwa jina la Musa Silvester anayedaiwa kupigwa Kwa kutumia kipande Cha nondo kichwani wakati akiamua ugomvi baina ya askari Polisi na Mgambo waliokuwa wakimshambulia kaka yake ambaye alikamatwa na mgambo akiuza samaki Kwenye chumba chake maarufa kama bucha ya samaki.

Kijana huyo amesema kuwa alikuta Askari Polisi pamoja na Mgambo wakiwa wamemshika Kaka yake ambaye alikuwa na panga ambalo anakutumia kukata samaki,lakini Kwenye purukushani panga hilo likamjeruhi mikono askari polisi na Mgambo akanyanyua nondo na kumpiga kichwani na kumsababishia majeraha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita  Kamishna Msaidizi Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi wa matukio hayo yote mawili ili kupata ukweli.

Kamanda Mwaibambe amesema kuwa askari linamshikilia Bahati Mkingwa (33)  aliyekuwa anauza samaki mkazi wa mtaa wa Mwatulole kwa tuhuma ya kumjeruhi askari G.3705 CPL Abel .

Amefafanua kuwa mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake ambao bado wanaendelea kutafutwa wanatuhumiwa kuwashambulia na kuwazuia kufanya kazi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top