Na;Ezekiel Kamanga
Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mbeya imeaanza kusikiliza kesi namba 3/2022 na kesi namba 14/2022 inayohusu mgogoro wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Konde mei 31,2022 baada ya kuahirisha mei 18,2022 kupisha mazungumzo baina ya pande mbili zinazopingana.
Awali Jaji James Karayemaha alitoa nafasi kwa pande mbili zinazopingana ili kueleza utekelezaji wa mazungumzo baina ya pande zinazopingana ambapo upande wa mleta maombi Askofu Dkt Edward Mwaikali ukiwakilishwa na Wakili Wliliam Mashoke na upande wa mjibu maombi umewakilishwa na Wakili Daniel Pallangyo.
Wakili William Mashoke ameiambia mahakama kuwa agizo lililotolewa mei 18,2022 la kuwakutanisha wadau wa pande mbili limefanyika mei 26 na mei 30,2022 na kuzikutanisha pande mbili lakini kutokana na changamoto za uchaguzi wa TLS Arusha walipokutana huko upande wa mjibu maombi walifika mawakili lakini katika mazungumzo upande wa Mawakili hawakuwa na uamuzi wa mwisho hivyo kuomba wakutane mei 30,2022 ukumbi wa GR City Hotel majira ya saa nane mchana lakini hawakuweza kukutana muda huo na kuomba wakutane jioni ya saa 11 jioni.
Hata hivyo majira ya jioni walipokutana na Mawakili wa wadaiwa,wadaiwa hawakufika walitoa udhuru lakini wakakubaliana kuendelea na kikao hicho ambapo hoja zizizojadiliwa ni pamoha na upande wa mleta maombi kuomba kugawanywa kwa Dayosisi mbili Mashariki na Magharibi pia kusitisha uapisho wa Askofu mteule jambo ambalo mawakili hawakukubaliana nalo walidai wao siyo waamuzi wa mwisho.
Kutokana na sula hilo kushindwa kupata ufumbuzi nje ya Mahakana naiomba mahakama isikilize hoja za mleta maombi kwa haraka kutokana na maslahi mapana ya waumini ikizingatiwa kila upande una maeneo unakokubalika na wafuasi wake.
Kwa upande wa mjibu maombi wakiwakilishwa na Dkt Daniel Pallangyo umeiambia mahakama kuwa mleta maombi ndiye hakufika kwa wakati kwenye kikao na viongozi wa serikali hawakushirikishwa na hawakupata taarifa yoyote na kwamba mleta maombi ndiye amekwamisha muafaka pia amepinga hoja za mleta maombi za kugawanya Dayosisi sambamba na kuzuia uapisho.
Baada ya Jaji James Karayemaha kuzisikiliza pande zote awali amesikitishwa na kitendo cha pande zote kushindwa kufanya maridhiano licha ya kupewa muda mrefu sababu zilizotolewa na pande zote hazina mashiko ukizingatia namna jamii inavyosubia kupatikana suluhu juu ya mgogoro huo.
Jaji Kareyemaha amesema hapakuwepo na juhudi za wahusika kuumaliza mgogoro huu badala yake mawakili ndiyo pekee waliokuwa wakikutana mara kwa mara licha ya msukumo mkubwa kutoka kwa waumini na pande zote zingetanguliza umoja na upendo.
Pia amesema pande zote zimeidanganya mahakama kwa kuwa hapakuwepo na ushirikishwaji wa viongozi wa serikali na tangu kutolewa muda wa mazungumzo viongozi wa serikali wahakushirikishwa.
Jaji aliahirisha kwa muda kikao cha mahakama majira ya saa 6:30 hadi saa 7:45 ili kutoa nafasi kwake kuweza kupitia hoja za pande zote zinazopingana na kutolea uamuzi.
Baada ya kurejea Jaji alimkaribibisha mleta maombi kutoa hoja ambapo Wakili Godwin Mussa Mwapongo anayemwakilisha mleta maombi ameomba Wakili Azael Mwaiteni na Benjamin Bembela kwa kuwa wao ni waajiriwa wa taasisi na kwamba wao wanaweza kuhitajika mahamani kutoa ushahidi sambamba na kuitafsiri katiba ya Dayosisi ya Konde na kwamba wanayo maslahi katika kesi hii.
Wakili Mussa aliongeza kuwa mawakili hao wajitafakari kama wanastahili kuwatetea wadai au la?,aidha Wakili Benjamin Mbembela hakupaswa kulisimamia shauri hilo kwa kuwa mwajiri wake ni mleta maombi katika shauri hili.
Hoja hizo zimepingwa na Wakili Azael Mwaiteni kwa kusema kuwa yeye anayo haki ya kuwatetea wadaiwa kwani ni sehemu ya wajibu wake licha ya kuwa ni mwajiriwa wao.
Naye Wakili Peter Kilanga amesema hoja zote zilizotolewa na mdai hazina mashiko hivyo mahakama itupilie mbali hoja hizo.
Wakili Dkt Daniel Pallangyo amesema hana pingamizi la kuendelea na shauri hivyo kuiomba mahakama isikilize na kutoa uamuzi mapema iwezekanavyo.
Jaji Karayemaha kwa kuzingatia uzito wa shauri lililopo mahakamani amekubaliana na hoja ya Wakili Mussa ya Wakili Mwaiteni na Mbembela wajitafakari kama ni sahihi kuwakilisha wadaiwa namba 4 na 5.
Aidha Jaji Karayemaha amekubaliana kuendelea kwa mashauri yote mahakamani na kwamba Amesema shauri liendelee kusikilizwa licha ya kutokuwepo kwa mdaiwa namba 14 Tusajigwe Boniphace na mdaiwa namba 26 Umilata Chaula ambao licha ya kupelekewa wito wa kuitwa kwenye shauri walikaidi kusaini na hawakufika mahakamani.
Wakili Ramsey Mwamakamba anayewatetea wadaiwa namba 6 hadi 29 amesema hana pingamizi lolote.
Upande wa mdai umeomba kusitishwa kwa uapisho wa Askofu juni 5,2022 pia ukiukwaji wa katiba ya Dayosi ya Konde amesema atayasikiliza masauri yote kwa pamoja.
Jaji ameahirisha shauri hilo hadi juni mosi,2022 saa 2:00 asubuhi atakapotoa uamuzi wa awali juu ya mawakili wanaodaiwa wajiondoe sambamba na kusikiliza mashauri yote mawili.