MKUU WA MKOA FEKI AKAMATWA MBEYA

0

Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia Wallen Mwinuka Mkazi wa Makondeko Jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 20 kwa tuhuma za kujifanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera kwa kutumia mtandao wa Instagram.


Mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 07, 2022 majira ya saa 08:00 mchana maeneo ya Mama John Jijini Mbeya

Akitoa taarifa Kwa waandishi wa habari Mkoani Mbeya Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina msaidizi mwandamizi wa Jeshi Hilo Ulrich Matei, amesema kijana huyo alifungua akaunti katika mtandao wa Instagram kwa Majina ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwahadaa watu kwa kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Kamanda Matei amesema kijana huyo ambaye amekua akijifanya Mkuu wa Mkoa na muda mwingine kuwa katibu wa Mkuu wa Mkoa alikua akinakili taarifa zake kutoka Ukurasa rasmi wa RC Homera na kuziweka kwenye Akaunti hiyo na pia alikuwa akitoa namba yake ya simu ili wananchi waweze kutoa kero au shida zao kwake na kukutana na watu mbalimbali wanaohitaji kuonana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera

Kijana huyo amesema alifungua ukurasa wa Instagram Kwa Kutumia majina ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kutokana na utendaji kazi wake Huku akiamini kufanya hivyo kunaweza mtengenezea nafasi ya kufanya kazi na Mkuu huyo wa Mkoa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top