Mkuu wa wilaya ya Lushoto Kalist Lazaro ameamuru kuwekwa rumande wakandarasi wa tatu Kwa kushindwa kukamilisha Kwa Wakati mradi wa Ujenzi wa barabara ya km 2.6 Kwa kiwango cha lami.
Uamuzi huo ameutoa leo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi ya barabara mkoa wa Tanga walipokuwa wakikagua mradi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Maguzoni hadi Bomani wilayani Lushoto.
Wakandarasi hao ni kutoka kampuni yaM/S KIV contractor,M/S HAMIERI.CO.LTD,M/S ANSIL ambao walitakiwa kujenga barabara ya kiwango chalami yenye urefu wa km 2.6 Kwa gharama ya sh Bil 1.2.
Amesema kuwa wakandarasi hao muda wao wa kukamilisha mradi walitakiwa kukamilisha kazi Toka Juni 19 mwaka huu lakini walishindwa kukamilisha Kwa wakati kazi hiyo .
"Nimeshindwa kuvumilia udanganyifu wenu Kila siku mnasema mnasubiri mirambo Kwa ajili ya kuweka lami Kwenye barabara hii lakini hakuna hatia zozote,hivyo mtakaa ndani mpaka hapo mtambo utakapofika ,nitawatoa Ili muweze kumaliza kazi hii"amesema DC Kalist.
Aidha amesema kuwa kuwakata fedha hao haiwezi kuwa sababu ya kukamilisha kazi Kwa wakati bali ni muhimu kuchukuwa hatuakali Ili mambo yaweze kwenda. Una maoni usisite kutuandikia