MORRISON; ATAJA KILICHOMUONDOA SIMBA,MKATABA MPYA CHANZO KUONDOKA

0

Hatimaye Benard Morrison aeleza kisa mkasa cha yeye kukataa kusaini mkataba mpya Simba Sc wakati mkataba wake ukiwa ukingoni kumalizika na wakati huu timu zikijiandaa na msimu mpya wa Ligi la Tanzania 2022/23.

Akifanya mahojiano Maalum na Global Tv  mchezaji, Benard Morrison, ametolewa majibu  masuala mbalimbali yanayomuhusu ikiwemo sababu za kuondoka Simba na klabu anayoelekea.


Morrison ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuitwa na Mkurugenzi wa Timu ya Simba kwa mazungumzo, ambapo anaamini kwamba madai aliyopewa na Mkurugenzi huyo hayakuwa na ukweli wowote ndani yake.

“Mkurugenzi aliniita ofisini kwake, nikaenda na ndipo aliponiambia kwamba wachezaji wenzangu wamekasirika na hawataki niendelee kuja mazoezini na makocha nao wanalalamika kwamba siwaheshimu, kwa hiyo malalamiko yamekuwa ni mengi kukuhusu.” Anasema Benard Morrison..

“Lakini nilisema hapana, mbona wachazaji hao hao ndiyo wanaonipigia simu mara kwa mara nisipoonekana mazoezini wakiniuliza naendeleaje? Jeraha langu linaendeleaje?” Anasema Morrison.

“Mwenyekiti wa Simba (Try Again) alikasirika sana baada ya kuona ile post kwamba naenda nyumbani kwa mambo ya kifamilia akaniambia hapana usiende nyumbani rudi kambini na uanze mazoezi na wachezaji wenzako”

“Nikamwambia hapana siwezi maana nimeshapost naondoka na Klabu imeshapost, kwa ninachojua mimi mwenyekiti alikuwa hajui chochote kuhusu mimi kutolewa kwenye Klabu,” Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison.

“Katika mkataba wangu mpya mshahara wangu ulipunguzwa sana, watu wengi wanasema vibaya kuhusu mimi, wanasema mimi ndio sababu ya Simba kuniacha ndio maana nimeamua kuongea.

“Fedha yangu ilipunguzwa sana kutoka kwenye mkataba wangu wa kwanza, nikawauliza kama huduma yangu sio muhimu na sifanyi vizuri ndani ya klabu basi mniache niondoke kuliko kupunguza mshahara maana inaonyesha sifai kupokea fedha niliyokuwa napokea awali hivyo nilikataa kusaini mkataba,” Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison.

“Walinipa mapumziko maana nilikataa kusaini mkataba mpya, kama ningecheza Simba miaka 5 au 10 alafu mwisho wa siku nikarudi Ghana sina hela au kumpgia mwenyekiti naomba hela kuisaidia familia yangu sio kitu kizuri”

“Niliomba mkataba mzuri, maboresho kwenye mkataba ili niwe vizuri kuihudumia klabu na haikufanyika hivyo, nilikuwa na kikao na Barbara na sababu Ya hicho kikao ni kwa sababu tulicheza mechi dhidi ya Yanga na ile mechi nilipata majeraha na awali tayari nilikuwa majeruhi kwenye mechi dhidi ya Orlando Pirates”

“Baada ya mechi daktari hakunifuata kunihudumia wala kujua hali yangu, nilimtumia meseji nyingi kuwa sipo sawa lakini hakufanya hivyo, niliwaambia hamnijali hivyo nililazimika kujihudumia mwenyewe nikiwa nyumbani”

“CEO alinipigia simu nikaenda ofisini kwake akaniambia wachezaji wanahasira, wanasema hawataki niende tena kambini wala mazoezini, kocha analalamika siwaheshimu, hawataki niende mazoezini hivyo malalamiko ni mengi ni kwa nini nafanya hivyo ?”

“Nilimjibu sio kweli sidhani kama wachezaji wanaweza kufanya hivyo maana ndio hao hao wachezaji wananipigia simu nisipoonekana kambini kunijulia hali lakini wewe CEO unasema hivi, Bocco, Mkude, Chama, Bwalya walikuwa wananijulia hali kila siku,” Mchezaji wa Simba Sc, Bernard Morrison.

TAZAMA VIDEO HII KUTOKA MKOA WA NJOMBE JUU YA MAFANIKIO YA ZAO LA PARACHICHI.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top