MTOTO ASAFIRI KM 430 AKINING'INIA KWENYE TAIRI UVUNGUNI MWA BASI

0

Mtoto mmoja wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 13 ameokolewa baada ya kusafiri umbali wa kilomita 430 kwa kujificha uvunguni mwa basi kwenye tairi la spea.

Mtoto huyo (jina limehifadhiwa) amesema siku ya kwanza alikuwa na mwenzake na walitembea kwa miguu kutoka Mtwara hadi kijiji cha Ndumbwe, na baada ya kuona hawafiki Dar es Salaam waliamua kurudi Mtwara.

Amesema siku iliyofuata akaamua kusafiri peke yake kwa kufika kituo cha mabasi cha Mtwara eneo la Mkanaledi na kwenda kujificha kwenye uvungu wa basi kwa kukaa kwenye tairi la spea, ambapo basi hilo lilikua likielekea mkoani Dar es Salaam.

Dereva wa Basi hilo Rashid Shamte amesema walitoka Mtwara majira ya maa moja kamili asubuhi  kuelekea Dar es Salaam na walipofika eneo la Bungu kijana mmoja aliyekuwa pembeni mwa barabara aliona miguu ya mtu ikining’inia na hivyo kutoa taarifa kwa dereva.

Dereva Rashid amesema baada ya kusimamisha basi abiria wote wakashuka baada ya kusikia chini ya basi kuna miguu ya mtu inaning’inia na walipoenda uvunguni mwa gari wakamkuta mtoto huyo na kuamua kusafiri naye hadi Dar es Salaam na siku iliyofuata wakarudi naye Mtwara.

Juhudi za kuwapata wazazi wa mtoto huyo zimeshindikana kwa kuwa wako nje ya mkoa wa Mtwara na kwa sasa mtoto huyo amekabidhiwa kwenye kituo cha polisi cha Mtwara kwa hatua zaidi.

Credit;TBC

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top