MTOTO WA RAIS AAPISHWA KUWA MAKAMU WA RAIS

0

 

Mtoto wa Rais wa Ufilipino anayeondoka madarakani Rodrigo Duterte, Sara Duterte ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Sara Duterte (44), binti wa Rais Rodrigo Duterte ameahidi kuwaunganisha Wafilipino, katika hafla ya kuapishwa kwake mjini Davao.

“Mimi sio bora au mtu mwenye akili zaidi Ufilipino na ulimwengu lakini hakuna mtu anayeweza kushinda uimara wa moyo wangu kama Mfilipino,”  amesema Duterte, ambaye alivaa gauni la kitamaduni la kijani.

“Sauti ya Wafilipino milioni 32.2 ilikuwa kubwa na ya wazi – yenye ujumbe wa kutumikia nchi yetu,” Duterte alisema, akimaanisha kura alizopata huku akipigiwa makofi kutoka kwa maelfu ya wafuasi wake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top