MUME ATUHUMIWA KUMUUA MKEWE BAADA YA KWENDA KUNYWEA PESA YA MAUZO YA MBUZI

0
Wahenga wanasema pata hela tujue tabia yako,sasa huko nchini KENYA Mzee wa miaka 70 anadaiwa kumchoma kisu mkewe hadi kupelekea kifo baada ya kutofautina kuhusu KSH.6000 za mauzo ya mbuzi wao.

Imeelezwa kuwa Marehemu aliyekuwa na umri wa miaka 42,alitoweka nyumbani baada ya kupata malipo ya mbuzi waliyouza siku chache kabla ya mkasa huo.
 
Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Embu Mashariki mwa Kenya Benjamin Muhia amesema baada ya kutoweka, mwanamke huyo alirejea nyumbani akiwa mlevi bila senti hata moja ya mauzo.

 Chifu wa kijiji cha Thau Daniel Ndwiga alisema alipata taarifa ya tukio hilo majira ya saa kumi na mbili jioni na alipofika eneo la tukio aliwakuta majirani waliokuwa na hasira wakipanga kumuua mshukiwa  (mumewe).

 Majirani wa wanandoa hao walisema walikuwa na mizozo ya nara kwa mara na hata wiki jana walikuwa na kesi katika katika ofisi ya Chifu wa eneo hilo na sasa Mtuhumiwa  yupo mikononi mwa Jeshi la Polisi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top