Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linaendelea na uchunguzi wa chanzo cha kina kifo cha mwalimu wa shule ya sekondari morogoro Daud Senyagwa kilichotokana na nyumba aliyokua alimokuwa amelala kuteketea kwa moto
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoa wa Morogoro Ralph Meela amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa seminari kata ya kingolwira Manispaa ya Morogoro.
Meela ameeleza kuwa bado wanaendelea baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifika mara Moja eneo hilo ambapo walikuta mlango upo wazi funguo za nyumba na gari zikiwa zinang'ing'ia mlango huku nyumba ikiwa imeteketea kwa moto na walipoingia ndani walikuta mwili wa Mwalimu Daud ukiwa sehemu alipokuwa amelala.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa amesema mwalimu huyo hakuwa akiishi hapo siku nyingi huku akieleza namna tukio hilo lilivyotokea.