MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA ALIYEPEWA UJAUZITO MWAMBE PEMBA AJIFUNGUA.

0
 Na, Hassan Msellem, Idawaonline.com, Pemba.
Mwanafunzi wa darasa la Saba (7) mwenye umri wa miaka kumi na saba (17) jina limehifadhiwa ambaye March 27, 2022 aligunduliwa kuwa na ujauzito wa miezi Saba nusu huko  Jombwe Mwambe Kisiwani Pemba, amejifungu Mtoto wa kike baada ya miezi tisa ya ujauzito kukamilika. 
Picha kutoka Maktaba
Akizungumz na idawaonline.com Mama mzazi wa Mtoto huyo amesema Binti yake aliyekuwa akisoma darasa la Saba (7)  ambaye inadaiwa alipewa ujauzito na Kijana aitwaje Makame Omar Bakari 30, tarehe 10 mwezi May amejifungua salama baada ya kuulea ujauzito huo kwa kipindi cha miezi tisa (9).
 
Amesema licha ya kuripoti Kituo cha Polisi Kengeja kuhusiana na tukio Hilo hakuna hatua yoyote ambayo ilichukuliwa Kwa ajili ya kumtia mtuhumiwa mbaroni.
"Tulitoa taarifa Kituo Cha Polisi Kengeja pamoja na Kituo Cha Polisi Madungu Chake Chake lakini Hadi hii Leo Mtoto wangu anajifungua" alisema Mama huyo
 Aidha amesema hali ya mama mzazi pamoja na kichanga hicho zinaendelea vizuri hadi muda huu.
 
BABA MZAZI WA BINTI ALIYEJIFUNGUA
 Nae Baba mzazi wa binti huyo amesema wamesikitishwa na kitedno cha binti yao kukatishwa masomo nakuomba mtuhumiwa kuchuliwa hatua kali za kisheria wakati atakapotiwa mbaroni.
‘’kwakweli suala hili limetusikitisha sana kwasababu mtoto wetu bado ni mdogo sana alitakiwa sasa hivi awe anaendelea na masomo lakini amekatishwa masomo pamoja na ndoto zake” ameleeza
JESHI LA POLISI MKOA WA KUSINI PEMBA
idawaonline.com ilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Richard Tadeo Mchomvu ili kufahamu juhudi walizochukua ili kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo lakini hakuweza kuweka wazi hatua wazochukua za kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.
MSAIDIZI WA HUDUMA ZA SHERIA WILAYA WILAYA YA MKOANI.
Bimkubwa Mohammed Ali ni msaidizi wa huduma za sheria Wilaya ya Mkoani na mwanaharakati wa wanawake na watoto, amesema kutokuchukuliwa hatua Kwa watuhumiwa wa Vitendo vya udhalilishaji ni Moja miongoni mwa sababu zinazopelekea vitendo hivyo kuongezeka
"Tunaposema vyombo vya Sheria ni pamoja na Jeshi la Polisi pamoja na madawati ya jinsia lakini mpaka sasa hivi wako kimya hakuna hatua ambayo wamechukua, kwahivyo ni kama limepuuzwa upande mmoja" aliongeza
MAJIRANI WA MSICHANA ALIEJIFUNGUA
Nao majirani wa Binti huyo wamesema kitendo Cha Binti huyo kupewa ujauzito kimewahuzunisha sana ukizingatia Bado Binti huyo ni mdogo na anaendelea na masomo.
"Kwakweli tumehuzunishwa Sana suala hili maana kwanza huyu mtoto bado ni mdogo sana na anasoma darasa la Saba, kwahivyo ameshamkatisha ndoto zake alizokuwa nazo Kwasababu hawezi kusoma huku ana ulezi wakati yeye mwenyewe bado ni mtoto labda anaweza kuendelea na masomo akishamuachiza" walisema majirani hao
MWALIMU MKUU WA SKULI YA MSINGI MWAMBE 
Ali Mohammed Omar ni mwalimu wa Skuli ya msingi Mwambe ambayo alikuwa anasoma msichana huyo, amekiri kupokea taarifa za binti huyo kujifungua na kutoa taarifa hizo kwa afisa mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba.
Aidha amesema binti huyo alikuwa ni mwanafunzi mtulivu, mpole na mwenye kufuata taratibu zote za skuli na alikuwa na ufahamu wa wastani.
KAULI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR
Mohammed Nassor Salim ni afisa mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba, amekiri kupokea taarifa za kujifungua kwa mwanafunzi huyo aidha amesema baada ya kumaliza siku arobaini (40) ya kujifungua anaweza kuendelea.
TAKWIMU ZA WANAFUNZI WALIODHALILISHWA NA KUPEWA UJAUZITO KUANZIA JANUARY HADI JUNE, 2022. 
Takwimu zilizotolewa na wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Kisiwani Pemba, zinasema takriban wanafunzi 11 wa Sekondari waliripotiwa kupewa ujauzito sita (6) kati ya wanafunzi hao wanaendelea na masomo na watano (5) wameacha.
Kwa upande wa wanafunzi wa skuli wa msingi waliopewa ujauzito ni wawili (2) waliolawitiwa ni wanne (4) na waliodhalilishwa ni mmoja (1).
Habari ya msichana huyo mwenye umri wa miaka kumi na saba (17) aliekuwa akisoma darasa la saba (7) kukutwa na ujauzito miezi saba na nusu ziliripotiwa katika kipindi cha Mawio March 27, 2022.
KAMA HUKUTAZAMA AVIDEO HII BASI USIPITWE ITAZAME KWA SASA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)


#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top