MWANAMKE ALIYEPOTEA MIAKA 5 ILIYOPITA MWILI WAKE WAKUTWA KISIMANI WAKATI WAKISAFISHA

0

 Polisi katika kaunti ya Trans Nzoia wanachunguza kifo cha mwanamke aliyetoweka mwaka wa 2017, na mwili wake kupatikana ndani ya kisima.

Wakaazi wa kijiji cha Rafiki kaunti ya Trans Nzoia wamepatwa na Butwaa baada ya kubaini kuwa wamekuwa wakinywa maji kutoka kwenye kisima kimoja ambacho kilikuwa na mwili .

Ripoti ya runinga ya Citizen ilionyesha kuwa kijana mmoja alikuwa ameajiriwa kusafisha kisima hicho baada ya kukauka, lakini alitoka humo akiwa na kiwewe akisema alikuwa ameona mwili.

"Siku zote tunajua mama alipotea,lakini hatukujua alikokwenda, Tulikuwa tukiambiwa tu kwamba alipotea," mmoja wa binti za mwanamke huyo alisema.

 "Hatuna maji katika eneo hili kwa hivyo tuliamua kusafirisha kisima kilichokauka maji ili tupate maji lakini tukaona mifupa'aliongeza.

 Kulingana na jamaa mwingine, kijana huyo alipatwa na kiwewe, akisema hataingia tena ndani ya kisima hicho, zaidi akibaini kuwa kulikuwa na mwili

Juhudi za kumtafuta mwanamke huyo alipotoweka mwaka 2017 ziligonga mwamba kwani waliweza kumtafuta huku wakati fulani wakiamini kuwa alikuwa akiishi na mwanaume mwingine.

 Kwa sasa polisi wanachunguza kubaini kilichomuua mwanamke huyo na kuthibitisha kupatikana kwa mwili wa mwanamke huyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top