NGOSHA AMUA MPENZIWE KISHA KUJIUA KWA SUMU DAR

0

 



Marehemu Bunanzi Kulwa

KATIKA hali ya kusikitisha Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Bunanzi Kulwa maarufu kama Ngosha Mkazi wa Mbagala kwa mbiku jijini Dar es salaam anadaiwa kumuua mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Happines Zakarika kisha nae kujiua kwa kunywa sumu, huku chanzo kikiwa bado hakijajulikana.

Tukio liho limetokea Juni 8 mwaka huu, huku likizua sintofahamu kwa majirani wa eneo hilo kutokana na marehemu hao kuishi kama dada na kaka kwa takribani miaka 2.

Waandishi wetu Issa mnaly na Richard Bukos (Globalpublisher) wamefika eneo la tukio na kuzungumza kwa kina na Rafiki wa karibu wa Marehemu Ngosha aliyejitambulisha kwa jina la Shineneko Ruge ambaye anabainisha kuwa marehemu alikuwa ni rafiki yake wa karibu.

Ruge amesema kuwa usiku mmoja kabla ya kifo cha marehemu alimpigia simu mama yake mzazi na kumuambia kuwa atajitoa uhai.

Aidha Ruge amebainisha kuwa siku moja kabla ya kufariki alikuwa na rafiki yake huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na moja kati ya maongezi yao ni kwamba alimuaga kuwa atasafiri yeye na dada yake kwenda Marekani hivyo alikuwa akifuatilia masuala ya Visa, lakini Ruge anasikitika kwa kusema kuwa hakufahamu kama hiyo ndiyo ilikuwa safari yake ya mwisho hapa duniani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top