katika hali ya kusikitisha mtoto wa miaka miwili Nkiya Thomas Bulandash amekutwa amechinjwa na watu wasiojulikana kutupwa kwenye samba la uwele karibu na nyumbani kwao.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nyamigogwa kata ya Shabaka Wilaya ya Nyang'wale mkoani Geita ambapo mkuu wa wilaya hiyo amelaani vikali tukio hilo na kusema linahusishwa na imani za kishirikina.