UKATILI; NELSON AKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA KICHWA

0

 Watu wenye silaha Kusini Mashariki mwa Nigeria wamemuua kwa kumkata kichwa mwanasiasa mwingine katika jimbo la Anambra.


Msemaji wa polisi, Ikenga Torchukwu ameiambia BBC kuwa mwili wa Nelson Achukwu- mbunge wa zamani katika jimbo la Anambra ulipatikana Jumanne baada ya kutekwa nyara kutoka nyumbani kwake mapema mwezi huu.

Haijabainika ni nani aliyetekeleza utekaji nyara na mauaji ya mwanasiasa huyo mlemavu.

Ripoti zinaonyesha kuwa ilikuwa ni mara ya pili yeye kutekwa nyara katika miezi kadhaa na pesa ililipwa ili kuachiliwa wakati wa kutekwa nyara kwake mara ya kwanza.

Achukwu alikuwa mwanasiasa wa hivi karibuni kulengwa katika eneo hilo.

Mamlaka mara nyingi zimewalaumu watu wanaotaka kujitenga wanaodai jimbo lililojitenga la Biafra kwa ghasia zinazozidi kuwa mbaya kusini mashariki mwa Nigeria.
Credit-BBC
TAFADHALI KABLA YA KUSOMA HABARI NYINGINE TAZAMA VIDEO HII ITAKUSAIDIA.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top