Jeshi la polisi Mkoa wa Nkombe limesikitishwa na vitendo vya wazazi kuendelea kuwanyanyasa watoto hali inayochafua taswira Mkoa wa Njombe.
Akizungumza kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah mbele ya waandishi wa habari ofisi wake amesema kuna watoto watatu wameokotwa kwa nyakati tofauti mkoani njombe.
"Tumeokota watoto watatu kwa muda mfupi kwa maeneo tofauti,kuna mtoto ameokotwa kwenye basi akiwa amevilingishwa na kitovu hakijakatwa,iligundulika kuwa na mtoto wakati basi hilo likienda kufanyiwa usafi na basi hilo lilikuwa likitokea lugalawa wilayani Ludewa kwenda Njombe mjini sasa hivi anaendelea vizuri yuko kibena hospitali' amesema kamanda Issa.
Katika tukio la pili kama amesema kuna mtoto ameokotwa kwenye shamba la mahindi eneo la mjini mwema mjini njombe.
'Ilikuwa inasikika sauti ndogo inalia kwenye shamba la mahindi watu walisambaa na ikaonekana ni mtoto ametelekezwa na mtoto huyo anaendelea vizuri na afya yake" amesema kamanda.
Katika tukio la tatu amesema mama mmoja amejinyonga baada ya kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa kuwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi.
'Kuna watoto wanazaliwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi eneo la Lupembe,mama baada ya kujifungua mtoto kama huyo amejinyonga,sasa kwa hali hiyo wewe uliyezaa unajinyonga wale watakao kaa nae itakuaje,mtoto kama huyo anaweza kulelewa na taasisi au serikali' amesema kamanda Issa.
Aidha amewataka wanawake wasiwe na mioyo ya ukatili kiasi hicho dhidi ya watoto wao.
TAZAMA KAULI YA KAMANDA ISSAH AKIZUNGUMZIA MATUKIO HAYO!