MFIWA ANASURIKA KICHAPO AKIMZIKA MUMEWE!

0

 Ester Mganwa mkazi wa mtaa wa Kilimahewa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,amenusurika kipigo kutoka kwa waombolezaji katika msiba wa mume wake Juma Mandoo wakimtuhumu mwanamke huyo kutenda kosa la kumtoroka marehemu mume wake akiwa mgonjwa na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine.


Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Ludewa katika mazishi ya mwanaume huyo bwana Linus Malamba ambaye pia ni kaimu katibu tawala wa wilaya ya Ludewa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

“Kilichotokea ni kwamba yule mama hakujitokeza mumewe alipofariki kwasababu alikuwa ameolewa na mtu mwingine,kwa hiyo umati wa wanawake waliona wamezalilishwa na yule mwanamke mwenzao kwa kitendo cha kutelekeza mgonjwa na mwili wa marehemu ndio maana wakaanza kumuazibu pia kwa kummwagia unga”Alisema bwana Mlamba

 

Hata hivyo amesema viongozi mbali mbali wakiwemo wa dini na serikali waliweza kukaa na wanawake waliotenda makosa hayo kwa mfiwa mwenye mtoto mmoja kwa kuwa aliomba radhi kutokana na makosa yake huku akitoa wito pia kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi.


TAZAMA VIDEO HII KILICHOJILI MSIBANI BAADA MKE KWENDA KUOLEWA AKIMTELEKEZA MUMEWE.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top