VIJANA 17 WAKUTWA WAMEKUFA KATIKA KLABU YA USIKU

0

 Polisi nchini Afrika Kusini imesema takriban vijana 17 wa umri wa kati ya miaka 18 na 20 wamekutwa wamekufa katika klabu moja ya usiku katika kitongoji kilichopo katika mji wa kusini mwa taifa hilo wa East London. 

Mkuu wa polisi katika eneo hilo brigedia Thembinkosi Kinana ameitaja klabu husika kuwa ni Scenery Park, ingawa pia amesema wanaendelea na uchunguzi wa kufahamu chanzo cha vifo hivyo.

Picha ambazo hazijathibitishwa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha miili isiyo na dalili zozote za majeraha, ikiwa imetapakaa kwenye sakafu ya klabu.

Televisheni moja nchini Afrika Kusini ilionyesha maafisa wa polisi wakijaribu kutuliza umati wa watu waliokusanyika nje ya klabu hiyo katika mji huo uliopo katika mwambao wa Bahari ya Hindi, takribani kilomita 1,000 kusini mwa jiji la Johannesburg.

TAFADHALI TAZAMA VIDEO HII YA APP 5 MUHIMU UNATAKIWA KUWA NAZO KWENYE SIMU


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top