Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kufanya uchunguzi dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma kutokana na ujenzi wa matundu 9 ya vyoo kwa shilingi milioni 26 katika shule ya msingi Mamongoro halmashauri ya mji wa Njombe.
Mkuu wa wilaya ametoa agizo mara baada ya kubaini mapungufu makubwa katika taarifa na BOQ ya ujenzi wa matundu 9 ya shule hiyo iliyopo kata ya Makowo.
“Matundu 9 ya vyoo ilitakiwa kujengwa kwa milioni 9 na laki tisa na ikizidi sana angalau itafika milioni 19 sio milioni 26.TAKUKURU wakifanya uchunguzi na ikabainika vinginevyo hatua zitachukuliwa”alisema Kissa Kasongwa
Mkuu wa wilaya anaendelea na ziara ya kupita kila kijiji katika halmashauri hiyo na kukagua kila mradi unaotekelezwa kwenye vijiji vya halmashauri hiyo.
TAZAMA KAULI YA DC HAPA AKIZUNGUMZA MWENYEWE