Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wameombwa kuandika habari zinazohusu maendeleo ya miradi ya Serikali inayotekelezwa kupitia fedha za UVIKO19 zilizotelewa kutekeleza miradi hiyo ili kufanya tathmini juu ya maendeleo ya miradi hiyo.
Akifungua mafunzo ya siku moja juu ya mchango wa mradi Uviko19 katika ustawi wa jamii pamoja na nafasi ya waandishi wa habari katika utekelezaji wa miradi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja huko Gombani Chake Chake Pemba, amesema utekelezaji wa miradi hiyo ya Uviko19 kwa kiasi kikubwa inategemea kalamu za waandishi wa habari katika kufuatilia na kuchambua maendeleo ya miradi hiyo.
‘’Sasa fursa ambayo tumeipata kwenye mfuko wa uviko19 ni kwamba kuna miradi ya maendeleo ina nafasi na fursa nyingi kwa waandishi wa habari ni sehemu ya kuanza kuichakata’’ alisema
Aidha amewaomba waandishi hao kujiongeza kitaaluma ili kuwa waandishi bora na wenye weledi katika utekelezaji wa majukumu yao sambamba na kusom fani maalum ambazo wataweza kuzifanyia kazi ipaswavyo.
“Uandishi wa habari imejigawa sehemu nyingi sana kuna mwandishi wa mambo ya mazingira tu, kuna mwandishi wa mambo ya afya tu huna unachoweza kumdanganya kwenye afya, kwahivyo soko la uandishi wa habari ni kubwa mno na haliwezi kujaa ni wewe kutambua uwezo wako uko wapi” alishauri
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, miongoni mwa dhamira ya Serikali katika utekelezaji wa miradi ya Uviko19 ni pamoja na ujenzi wa barabara za ndani zenye urefu wa kilometa 270 Unguja na Pemba ili kuwaondoshea wananchi changamoto ya usafiri.
“Kama tunavyofahamu miongoni mwa changamoto zinazowakabili wananchi wengi ni pamoja na ubovu wa barabara hususan barabara za ndani lakini kupitia fedha hizi za Covid19 Serikali imedhamiria kuzijenga kwa kiwango cha mali barabara za ndani zenye urefu wa kilometa 270 Unguja na Pemba” alisema Mkuu huyo
Amesema ujenzi wa hospitali kumi (10) kwa Wilaya zote za Zanzibar pamoja, uimarishaji wa vifaa kinga na tiba pamoja na kuajiri wataalamu wa Afya ni miongoni mwa miradi ya uviko19 ambayo kwa kiasi kikubwa itapunguza kadhia ya upatikanaji wa huduma bora za Afya Visiwani Zanzibar.
Nae, Afisa Mdhamin Ofisi ya Rais Ikulu Pemba, Shuweha Abdalla Omar, amesema ofisi ya Rais Pemba imeandaa utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwisho wa mwezi ili kujadili mafanikio na changamoto juu ya maendeleo ya miradi ya Uviko19 inayaendelea maeneo mbali mbali Nchini.
Akichangia mada mwandishi kutoka Jamii Online TV Ali Massoud Kombo, ametoa ushauri kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya kuongozana na wataalamu pamoja na waandishi wa habari pindi wanapokwenda kukagua miradi hiyo ili kutambua hali halisi ya maendeleo ya miradi hiyo.
“Niwaombe sana waheshimiwa munapokwenda kukagua hiyo miradi ya Covid naomba muongozane na wataalamu husika kwa mfano unakwenda kukagua vifaa tiba tafuteni mtaalamu wa vifaa tiba muende nae ili kujua ukweli juu ya vifaa tiba hivyo kama vina ubora ama laa’’ alitoa ushauri
Wakichangia mada waandishi kutoka vyombo mbali mbali vya habari wamesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni pamoja na maslahi duni ya mishahara na posho, jambo ambalo linapelekea kushindwa kufanyakazi kwa ufanisi.
‘’Tunakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo maslahi duni ya mishahara kwa wale ambao wameajiriwa kwa wale ambao hawaja ajiriwa wanalipwa posho ndogo sana, kwahivyo tunashindwa kufanyakazi kwa ufanisi kwa mfano mwandishi anataka aende sehemu Fulani kufanyakazi lakini hana hata nauli analala” alisema mmoja wa waandishi hao
Mfamau Hilal Mfamau ni Afisa Mdhamin Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Pemba, amewataka wanahabari hao kufanyakazi kwa bidii na kuwa wabunifu ili kuzalisha habari zenye kuibua mafanikio na changamoto mbali mbali katika jamii.
“Najua munakabiliwa na changamoto nyingi sana kama mulivyosema lakini munaweza kuzigeuza hizo changamoto kuwa fursa, niwaombe muendelee kufanyakazi kwa bidii pamoja na ubunifu naamini iko siku mutakuja kuyasahau haya munayoyalalamikia leo” alishauri.
Fedha za miradi ya UVIKO19 zimeelekezwa katika utekelezaji na uboreshaji miradi ya elimu, afya pamoja na maji.
Kupitia mfuko wa fedha za UVIKO19 jumla ya vyumba vya madarasa 208 yamejengwa pamoja na matundu ya vyoo 467 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba pekee, Wilaya ya Micheweni ikiwa na vyumba vya madarasa 77 na Wilaya ya Wete vyumba vya madarasa 131,
Kwa upande wa Mkoa wa kusini Pemba jumla ya vyumba vya madarasa madarasa 185 vimejengwa pamoja na matundu ya vyoo 222.
Mafunzo hayo ya siku moja juu ya dhamira ya Serikali na juhudi za waandishi wa habari katika kutangaza miradi ya UVIKO19 yameandaliwa na ofisi ya Rais Ikulu Pemba, yamejumuisha waandashi wa habari Kisiwani Pemba pamoja na Viongozi wa Serikali.
Maradhi ya UVIKO19 yaligunduliwa rasmi Disemba 2019 huko katika Mji wa Wuhan China ya kati baada ya kikundi cha watu kuugua homa ya Nimonia bila ya chanzo chake kueleweka na kubainika baadae kama aina mpya ya Virusi vya Korona.
Tarehe 20 Januari 2020 Waziri Mkuu wa China Li Keqiang alitoa wito wa kuongeza juhudi katika kukomesha na kuthibiti janga la nimonia lililosababishwa na virusi vya Korona, na kufikia March 23, 2020 kesi 337,000 zikathibitishwa rasmi.
![]() |
Ujenzi wa Soko la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Madungu Chake Chake Pemba. |