MJAJA; WAANDISHI ZIJUENI SHERIA ZA HABARI MUONGEZE NGUVU KUTETEA ZIFANYIWE MABORESHO

0

  Na, Hassan Msellem, Pemba- Idawa Online

Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kuzifahamu Sera na Sheria za habari zilizopitwa na wakati ili kuongeza nguvu katika utetezi na kufanyiwa marekebisho chanya.

Mapema akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari Kisiwani Pemba Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatibu Juma Mjaja, amesema waandishi wa habari ni wadau wakubwa wanaoweza kuleta mabadiliko ya Sheria za habari ambazo zinaonekana kukinzaba na uhuru wa habari na Wanahabari.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba Khatib Juma Mjaja akiwashauri Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba juu ya umuhimu wa kuzifahamu sheria mbali mbali ili waweze kuzifanyia utetezi.

Aidha mkuu huyo amewaomba waandishi hao kuzifahamu Sheria za mitandao ya kijamii pamoja na takwimu ili kuandika habari zenye ukweli na kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.

        “Kwahivyo wajibu wetu wanahabari nikuzifahamu sheria za habari mbali mbali wengi wetu tunafanyakazi na online media tunafanyakazi za takwimu, kwahivyo ni wajibu wetu kuzifahamu hizo sheria ili tufanye kazi zetu kwa ufanisi” alitoa ombi mkuu huyo 

Kwa upande wake Katibu Mtendaji kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga, amesema ili kuchochea nguvu ya marekebisho na maboresho ya Sheria kandamizi za uhuru wa habari wanahabari hawana budi kuzifahamu Sheria hizo.

        “Ni lazima wanahabari wazielewe sheria hizo kwasababu kuna usemi kwamba kutojua sheria sio utetezi pale unapoivunja walau wajue vifungu ambavyo vitawahusu mara Kwa mara” alitoa ushauri

Nae wakili kutoka Baraza la Habari Tanzania Mpale Mpoki, amesema ibara ya 18 ya katiba ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania na ile ya Zanzibar imeruhusu uhuru wa kutoa maoni, hivyo basi amesema uhuru wa kutoa maoni ni haki ya msingi ya mwanadamu licha uhuru huo kuminywa kwa baadhi ya wakati.

        “Uhuru wa maoni ni kitu cha msingi katika maendeleo na kutafuta ukweli na katika kuimarisha demokrasia na utawala bora” alieleza

 Shifaa Said Hassan ni Afisa program mwandamizi wa baraza la habari Tanzania upande wa Zanzibar, amesema Sheria ya mwaka 1988 ya wakala wa habari na magazeti ni Sheria inayokandamiza uhuru wa habari, hivyo basi amewataka waandishi hao kuendelea kufanya uchechemuzi katika kazi zao ili kuhakikisha mabadiliko katika sheria hizo yanafanyika.

  “Kwahivyo tukingalia tutaona kuwa sheria zimetungwa muda mrefu sana na haziendani tena na mazingira ya sasa katika tasnia ya habari kwahivyo wanahabari ni jukumu letu kuhakikisha tunashirikiana kuandika habari na kufanya vipindi ambavyo vitachochea kufanyiwa marekebisho chanya” alisema

Ameongeza kuwa bado kuna uminywaji mkubwa wa uhuru wa habari nchini kwa waandishi kutokuwa na uhuru wa kufanya kazi zao ipaswavyo ikiwemo kunyimwa taarifa, kupewa vitosho, kupigwa, kutekwa, kunyanyaswa kudhalilishwa pamoja kufungwa kwa vyombo vya habari.

        “Kama tunavyofahamu mara kwa mara tunapata taarifa za vyombo vya habari mbali mbali kufungiwa na baadhi ya wanahabari kupigwa na kudhalilishwa hii yote inatoa picha kuwa bado uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari hatujakuwa na uhuru wa kuridhisha katika utekelezaji wa majukumu yetu” aliongeza

Akitoa ufafanuzi juu ya tuzo zinazotelewa na baraza hilo Afisa programu kutoka baraza la habari Tanzania (MCT) Saumu Mwalimu, amewaomba wanahabari hao kuandika habari zinazogusa maisha ya wananchi nakuleta mabadiliko chanya katika jamii ili ziweze kuwa na vigezo vya kuchaguliwa kuwania tuzo hizo

“Kama tunavyojua kwamba baraza la habari Tanzania kila mwaka hua tuna mashindano ya kuwania tuzo katika categories mbali mbali hivyo basi niwasihi mufanye kazi zenye kuleta mabadiliko Fulani katika jamii na sio kuandika habari nani kasema ambazo hazimgusi mwananchi wa kawaida” alieleza afisa programu

Essau Kalikubira ni mwandishi wa UGA ONLINE TV, amesema sheria ya usimamizi wa vyombo vya habari vya mtandaoni ni sheria kandamizi kwani inanyima uhuru wa waandishi kuafanyakazi ipaswavyo, hivyo basi ameliomba baraza la habari Tanzania kuendelea kukutana na wadau wa Sheria ili kuifanyia marekebisho Sheria hiyo.

        “Kwakweli hii Sheria ya Mitandaoni bado naiyona ni Sheria kandamizi sana kwa waandishi wa habari wa mtandaoni kwasababu inamfanya mwandishi ashindwe kufanyakazi kwa ulaini na haraka kwani kila tukio inamlazimu kutoa taarifa kwa mamlaka husika ndipo aweze kufanyakazi” alisema

Nao waandishi hao wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo hayo na kuwa mabalozi wazuri kwenye vyombo vyao ili kuhakikisha wanafanyakazi kwakuzingatia Sheria pamoja na kuongeza nguvu katika uchechemuzi wa marekebisho ya Sheria hizo.

Bado Waandishi wa habari nchini Tanzania wanatumia Sheria kuu za habari ambazo ni Sheria Nambari 5, ya mwaka 1998 ya usajili mawakala wa habari, magazeti na vitabu na Sheria ya tume ya utangazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997 ambazo zinaonekana kuminya uhuru wa Habari na wanahabari.

Mwaka 2021, vyombo kadhaa vya Habari kama vile magazeti na runinga vilifungwa kwa nyakati tofauti pamoja na baadhi ya wandishi kunyanyaswa na kupigwa.

Miongoni mwa vyombo hivyo ni gazeti la Raia Mwema ambalo lilifungiwa kwa kipindi Cha Siku 30, gazeti la Uhuru siku 14, Wasafi TV miezi 6, kufungiwa Kwa Kipindi Cha Take One Cha Clouds TV kwa kipindi cha miezi 3 pamoja na kupigwa kwa mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi Zanzibar Josse Mikofu.

Mafunzo hayo ya Siku Moja yaliyojumuisha Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Baadhi ya Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wakiwa katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuhusu Sheria mbali mbali za Habari.

Afisa programu kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) akitoa ufafanuzi na historia kuhusu tuzo EjAT zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kila Mwaka

Afisa Habari kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Pemba Gaspery Charles Gaspery, akieleza jinsi alivyowahi kushiri katika tuzo za EJAT nakuibuka mshindi.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top