Wananchi wenye asili ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe wametakiwa kurejea nyumbani kuhesabiwa kwenye Sensa ya watu na Makazi agosti 23 2022 ili kuchochea maendeleo ya wilaya ya Makete.
Mh.Francis Chaula Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete |
Akizungumza
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Mh.Francis Chaula na mtandao huu Idawa Online amesema ili Wilaya ya Makete ipate mkate wa taifa mkubwa (Bajeti) serikali pamoja na mambo mengine itangaliwa idadi ya watu waliopo eneo husika hivyo niwatake wananchi wa wilaya
ya Makete waishio nje ya Makete warejee nyumbani siku ya agosti 22 wawe Makete
ili kesho yake wahesabiwe wakiwa nyumbani.
“Serikali
inapotengeneza bajeti au inapoleta maendeleo kigezo kikubwa lazima iangalie idadi
ya wananchi,kwamba kuna wakazi wangapi ili kusudi kuweza kuwaletea miradi ya
maendeleo,hivyo niwatake viongozi wenzangu,viongozi wa dini,Wanamakete
tusaidiane kuhamasisha wananchi tarehe 23 agosti wajitokeze kuhesabiwa” amesema
Chaula.
Mh
Chaula amesema Wanamakete lazima watambue kuwa ni muhimu kurejea nyumbani
kuhesabiwa ili kuchochea maendeleo.
Aidha
amesema kumekuwa na Maombi kwa serikali kugawa wilaya ya Makete kuwa na Majimbo
mawili ambapo amedai bila kuwa na idadi
ya kutosha hilo halitowezekana.
‘Watu
wanafikilia tugawe jimbo,hatuwezi kuwa na jimbo,hatuwezi kuwa na Halmashauri
mpya kama idadi ya watu ni ndogo’
Ikumbukwe
kuwa tarehe 23 agosti mwaka huu kila mtanzania anahimizwa kushiriki Sensa ya
watu na Makazi ili kupata takwimu sahihi za idadi ya watu pamoja na kutumika
kwa Takwimu hizo kupanga mipango ya kimaendeleo ya Taifa.