WANANCHI WACHOMA MOTO GARI LILILOUA MWENDESHA BODABODA

0

  

Na Victoria Robert , Kahama
Waendesha bodaboda pamoja na wananchi wenye hasira kali wamedaiwa kuchoma moto gari aina ya Noah lenye namba za usajili T 975 DHH na kusababisha uharibifu mkubwa wa gari hilo kuteketea kwa moto.

Hatua ya boda boda hao pamoja na wananchi ya kuteketeza gari hilo kwa moto imekuja baada ya mwenzao aliyefahamika kwa jina la Hiali Mgina (38) mkazi wa mtaa wa majengo wilayani humo kugongwa na gari hilo na kumsababishia kifo chake.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga George Kyando aliyasema hayo jana wakati akizungumza na michuzi blog kwa njia ya simu yake ya kiganjani.


Aidha Kamanda Kyando alidai kuwa tukio hilo lilitokea Juni 19,2022 majira ya saa nne usiku baada ya dereva wa gari hilo kumgonga mwendesha boda boda katika eneo la barabara ya uwanja wa Magufuli kuelekea Mhongolo hali iliyopelekea kifo chake hapo hapo.


Kufuatia tukio hilo mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga ametoa onyo kali kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto bila kuzingatia sheria ya usalama barabarani.


Marehemu Hiali Mgina ameacha mjane na watoto watatu huku mwili wake ukisafirishwa kuelekea Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top