WANANCHI WASEMA WANASHINDWA KUCHANGIA DAMU SABABU YA KUKOSA SUPU.

0

Na Henrick Idawa

Wananchi wilayani Makete Mkoani Njombe wamesema wanashindwa kuchangia damu kutokana na dhana zilizopo ndani ya jamii na kukosekana kwa elimu sahihi juu ya Uchangiaji wa Damu na matokeo baada ya kuchangia Damu.


Wakizungumza na Mtandao huu akiwemo Mama Raulia mkaazi wa  wilayani Makete Mkoani Njombe na Baraka Kemaia mkaazi wa Mbalali mkoani Mbeya waliofika kupata matibabu Ikonda Hospitali wamesema katika jamii wengi wao wanafahamu kuwa ukitoa damu inakupasa kulavyakula  Fulani ili kurejesha damu iliyotolewa na wengine wakiamini kuwa Ukitoa damu unatakiwa kila mwaka uwe unatoa Damu kwa sababu inakuwa inaongezeka kwa wingi mwilini.

‘Kwa kweli elimu ipite,tukipata elimu wengi tutachangia kwa kuwa hatujapata elimu ndio maana hatuoni umuhimu wa kuchangia damu’ amesema Baraka.

‘Wengi tunaogopa kuchangia Damu kwa sababu katika jamii unasikia wanasema ukichangia damu inatakiwa uwe unakunywa supu na vyakula vizuri vizuri kwa hiyo wanavyosema hivyo wengi tunaogopa kuchangia Damu’ amesema mama Raulia.

Mtandao huu umezungumza na Mkuu wa Idara ya Mpango wa Damu salama kutoka Hospitali ya Consolatha Ikonda Yusto Titusi Kyando amesema ni kweli jamii imekuwa na dhana potofu kuhusu uchangiaji wa Damu hali inayochangia jamii kuwa na mwitikio mdogo kuhusu kuchangia damu.

‘Miongoni mwa changamoto tunayokabiliana nayo ni jamii kuamini kuwa uchangiaji wa damu lazima awe na ndugu yake anayeumwa,wengine wanaamini ukichangia damu lazima uumwe kichwa mara kwa mara,na wengine kudhani lazima uwe na chakula maalum jambo ambalo sio sahihi’ amesema Kyando.

‘Wengi wanadhani uchangiaji wa damu lazima apate kitu kwa maana kwamba sisi kama wataalam tunapata faida tunapotoa kwa wagonjwa,hii inatuletea shida sababu mtu unapomuomba achangia damu anafikiri kwamba tutapata faida kwa kuiuza ile damu lakini damu kuchangia ni Bure na kuongezewa Damu ni Bure. Amesema Yusto Kyando.

Aidha amesema ni vyema jamii ikakubali maelezo na elimu inayotolewa na wataalam na sio elimu ya mitaani isiyo sahihi kwani watu wengi wanahitaji kuongezewa damu kila siku na hakuna ajuaye atahitaji Damu lini na wakati gani na kwamba suala la kuchangia damu linaufanya mwili kuwa na afya zaidi.

Kuhusu nani anapaswa kuchangia damu amesema kila mtu aliyefikisha umri wa miaka 18-60 anaweza kuchangia damu,awe na kiwango cha damu kinachohitaji mwilini kuanzia (Hemoglobin Level 12.5-18),uzito kuanzia Kg45 na kuendelea na wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Virusi vya UKIMWI hawaruhusiwi kuchangia damu,wanawake wajawazito & wanaonyonyesha hawaruhusiwi kuchangia Damu na wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya kurithi kama kifafa ,ugonjwa wa moja na siko seli hayo ni baadhi yanayozingatiwa kabla ya kuchangia damu.

Alipoulizwa kuhusu Kadi anayopewa mtu baada ya kuchangia damu Yusto Kyando  amesema kadi hiyo ni ishara ya kutengeneza familia ya uchangiaji  wa damu na kuwa balozi kwa jamii juu ya uchangiaji wa Damu na kwamba mtu mwingine anapoona Kadi hiyo anaweza kuhamasika kuchangia damu.

Raphael Luhanga ni Katibu wa Hospitali ya Consolatha Ikonda amesema hospitali hiyo kwa ukanda wa Nyanda za juu kusini mwa Tanzania imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kutokana na kuwepo kwa huduma nyingi za upasuaji wa kibingwa hali inayopelekea kuwa na uhitaji wa Damu ya makundi mbalimbali nyingi ili kuwasaidia wahitaji.

TAZAMA VIDEO HII WANANCHI WAKIELEZA KWA UNDANI NA WATAALAM WA AFYA WAKITOLEA UFAFANUZI

NB:Ikumbukwe kuwa zoezi la Uchangiaji wa Damu ni hiyari na muhimu kuchangia ili kuokoa maisha yaw engine bila Kutozwa garama ya uchangiaji au kuongezewa Damu katika hospitali zote hapa nchini,hivyo mimi na wewe ni sehemu ya jamii inayohitaji Damu tuunganae kuchangia damu katika vituo vya afya ili kuokoa maisha ya wapendwa wetu. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top