WATUMISHI WA UMMA LUDEWA WALIA NA UHAMISHO

0

Ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa kuanzia juni 16 -23 kila mwaka kote nchini katika kuadhimisha wiki hili, watumishi wilayani Ludewa mkoani Njombe wamelalamikia kutopewa uhamisho pamoja na kutolipwa fedha za likizo pindi wanapoomba.

Wakitoa malalamiko hayo watumishi wa baadhi ya kata ambazo afisa utumishi wa wilaya hiyo Gladness Mwano alipotembelea kata hizo akiwa ameongozana na baadhi ya watumishi wa ofisi yake kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali.

Hata hivyo Afisa utumishi wa wilaya hiyo Gladness Mwano amesema suala la kutotoa uhamisho ni kutokana na uhaba wa watumishi wilayani humo hivyo ni vigumu kuruhusu kuhama pasipo kuwa na mbadala wa mtu wa kuziba hiyo nafasi.

"Tumekuwa tukipokea maombi mengi ya kuhama pasipo kupata maombi ya watumishi kuhamia, hivyo tukiruhusu watumishi kuhama tutajikuta wananchi wanakosa huduma na tutazidi kupungukiwa zaidi na watumishi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top