Raia mmoja wa taifa la Nigeria atatumikia kifungo cha siku 30 gerezani iwapo atashindwa kulipa shilingi elfu kumi za kenya kwa makosa kumporomoshea matusi mpenzi wake na maafisa wa polisi walioingilia kumwokoa binti huyo.
David Olaydaju alipewa adhabu hiyo na Hakimu Mkuu Mkaazi wa Mahakama ya Kibera Philip Mutua baada ya kukiri makossa ya kusababisha usumbufu wenye uwezo wa kutatiza Amani.
Olaydaju alitekeleza makossa hayo eneo la Gathondeki mtaani Dagoretti katika Kaunti ya Nairobi mnamo Alhamisi, Julai 14, ambapo alimporomoshea matusi Edith Wachiria akitishia kumpiga.
Raia huyo wa kigeni alianza kumtukana mlalamikaji na majirani wake katika makaazi ya Hill View akitishia kumpiga, ambapo msichana huyo akikimbilia kwa walinzi wlaiomshauri kupiga ripoti kituo cha polisi.
Mahakama ilielezwa kuwa maafisa wa polisi waliingilia lakini Olaydaju aliendelea na vioja na matusi na kuwafanya maafisa hai kumtia mbaroni.
Walipeleka katika kituo cha polisi cha Kabete na kumwandikia mashtaka ya mienendo ya kukosea wengine na kusababisha usumbufu wakuhatarisha amani.
Olaydaju alisema kuwa alikuwa amekasirishwa na hatua ya mpenzi wake kumfungia katika nyumba hiyo kwa saa kadhaa na kuomba mahakama kumhurumia akielezea kukubali kukosea.
TAZAMA VIDEO HII UTAJIFUNZA JAMBO KATIKA HILI