WATU nane wamefariki dunia wakiwamo watano wa familia moja, kufuatia ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso usiku wa kuamkia Julai 11, 2022 katika eneo la Busiri barabara kuu ya kutoka Lusahunga kuelekea Nyakahura Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera.
Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema kuwa miongoni mwa watu hao nane waliofariki, wamo watano wa familia moja ambao ni mama na watoto wake wanne.
Kamanda Mwampaghale amesema kuwa ajali hiyo imeyahusisha gari la mizigo lililokuwa likitokea nchini Rwanda kwenda mkoani Dar es Salaam likiendeshwa na Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda na Toyota Succeed lililokuwa likitokea eneo la Nyamalagala wilayani Biharamulo kuelekea Benaco wilayani Ngara likiendeshwa na Nyawenda Bihela (35) ambaye nae aliyefariki katika ajali hiyo.
Amesema pia abiria wote waliokuwa katika gari aina ya Toyota Succeed waliopoteza maisha na kutaja majina yao kuwa ni Nyawenda Bisalo (35), Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo (6), Vedastina Sekanabo (8), Michael Charles (28) na Majaliwa Kanundo (32).
wa mujibu wa Kamanda Mwampaghale uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori kutokana na kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara na kuendesha gari upande wa kulia, na kusababisha magari hayo kugongana uso kwa uso. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika kituo cha afya Nyakanazi kilichoko wilayani Biharamulo
TAZAMA VIDEO HII ITAKUSAIDIA KAMA SI LEO KESHO