Mtayarishaji wa maudhui mwenye utata nchini Kenya Aq9ine kwa sasa amelazwa hospitalini akiwa katika hali mbaya baada ya kuripotiwa kula buibui.
Haya yanajiri baada ya Aq9ine Jumamosi, kuchapisha video inayoonyesha uso wake na mkono wake umevimba akiwaomba wafuasi wake wamwombee.
Katika video hiyo, alionekana kujikuna uso wake unaofanana na uvimbe na mikono iliyofunikwa na vipele, akitaja kama madhara ya kitendo chake cha kula buibui.
“Jamani fanyeni maombi yenu ya mwisho kabla niende. Mniombe tu bana mi naenda…Nasikia ni kama sina uso, nimefura kila mahali,nimekulaa buibui bana na hili linanitokea uso mzima,” alisema kwenye video hiyo.
Baadaye Aq9ine alijibu mapigo kutoka kwa baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii baada ya video hiyo kusambaa, akisema angesalia bila kuinama; zaidi hata kuongeza kuwa, akipona, atapika na kula chura na nyoka.
“Mnaboo bana..mnacatch juu ya mashida zangu why? Mimi nikikufa ntazikwa na mnisahau. Haufai kushtuka juu mimi si wenu.. Nikipona next ni chura na nyoka. Nlisema nitapika adi nikufe. I guess niko karibu.. Alichapisha.
“Uzuri wangu sitawai wapostia Till munichangie pesa ya hospital. Bora mnipromise nikikufa mtapull up kwa mazishi yangu Kenya mzima na msaidie familia yangu kupanga mazishi.”alinukuliwa