ALIYEMBAKA MTOTO WA MIAKA 6 MAHAKAMA YAMUANGUSHIA RUNGU LA MAISHA

0

 Mwanakulitafuta mwana kulipata,ndivyo unaweza kusema baada ya Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kumhukumu kifungo cha Maisha Bugingo Masatu(22) mkazi wa Mtaa Sedeko Mugumu kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka 6.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya Adelina Mzalifu,mwendesha mashitaka wa Jamhuri Renatus Zakeo katika kesi ya Jinai namba 22/2022 ameiambia mahakama kuwa,mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 7,2021 majira ya usiku nyumbani kwao na mtoto huyo.
Amesema,siku ya tukio mshitakiwa alikwenda kumtembelea rafiki yake ambaye ni baba wa mtoto huyo na kulala chumba cha watoto,ilipofika usiku wa manane alimbaka mtoto huyo na kumuumiza na kufanikiwa kutoroka alifajiri kabla ya wazazi hawajapata taarifa ya ukatili aliomfanyia mtoto huyo.
Zakeo amebainisha asubuhi mtoto alimwambia mzazi wake na kulazimika kutoa taarifa kituo cha Polisi Mugumu na kuanza kumsaka na walifanikiwa kumkamata baada ya siku kudhaa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kubaka mtoto ambalo ni kinyume na kifungu 130(1)(2)(e),131(3) kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2019.
Ameomba Mahakama itoe adhabu kulingana na hitaji la sheria kwa kuzingatia kosa aliloshitakiwa nalo.

Katika utetezi wake kabla ya kutolewa kwa hukumu Masatu ameomba Mahakama impunguziwe adhabu kwa kuwa yeye ndiye kijana mkubwa anayetegemewa kwao.
Hata hivyo utetezi wake haukuweza kuishawishi mahakama,ndipo Hakimu Mzalifu akasema,kulingana na kosa alilotenda na kwa hitaji la sheria adhabu yake ni kifungo cha Maisha na kuwa milango ya rufaa iko wazi.

UMETAZAMA VIDEO HII,AJIANDAA KUFA KWA KUKIUKA MASHARTI YA MGANGA.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top