AMVIZIA KISHA KUMBAKA NA KUMUUA MKE WA RAFIKI YAKE

0

 Polisi wanawashikilia wanaume wawili kuhusiana na mauaji ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 eneo la Mowlem, mtaani Umoja katika Kaunti ya Nairobi nchini Kenya.


Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI), Edwin Onditi Odada (mshukiwa mkuu) na Samuel Juma Otieno walinaswa Jumatano, Julai 20, kuhusiana na kifo cha Pamela Asesa.

 Ripoti ya DCI inasema kuwa Odada ambaye ni rafiki wa karibu wa mume wa marehemu, alifika  nyumba ya wawili hao na Pamela kumkaribisha huku mumewe ambaye ni mhandisi katika kampuni moja kwenye barabara ya Mombasa jijini Nairobi akiwa kazini.

Mshukiwa anaripotiwa kumbaka mke wa rafiki yake kabla ya kumuua kwa kumnyonga kutumia nguo ambayo pia aliijaza kwenye mdomo wa mwendazake kabla ya kufunga mlango na kutoroka.

Odada amekiri kutekeleza mauaji hayo mnamo Julai 12,2022 huku Otieno akiwa mshukiwa wa pili kwa kupatikana na simu ya marehemu. 

Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa mumewe alirejea nyumbani mwendo wa saa mbili usiku na kupata mlango wa nyumba yake umefungwa huku simu zake zikikosa kupokelewa.

 Aliomba usaidizi na kuvunja mlango huo ambapo alipigwa na butwaa baada ya kuona mwili wa mkewe ukiwa kitandani na kitambaa mdomoni. 

Washukiwa walikamatwa eneo la Tushauriane mtaani Kayole wakitarajiwa kufikishwa mahakamani na inaelezwa kuwa Kabla ya tukio hilo, mwanamke huyo aliwahi kumwambia mumewe kuwa rafiki yake alijaribu kumbaka.

 Mshukiwa alikuwa rafiki wa karibu wa mume wa mhasiriwa kiasi kwamba walikuwa wakiishi pamoja katika nyumba hiyo. Oduor hata hivyo alimtimua mshukiwa baada ya kuarifiwa na mkewe kuwa alijaribu kumbaka kisha baadaye akarejea kutekeleza unyama huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top