APELEKWA RUMANDE KWA TUHUMA ZA KUBAKA MARA MBILI.

Hassan Msellem
0

Mahakama ya Mkoa Chake Chake imempeleka rumande Mudrik Mohammed Kumbe mwenye umri wa miaka 18 Mkaazi wa Kinyasini Mkoani kwa tuhuma za kum'baka mara mbili msichana mwenye umri wa miaka 16.


Ilielezwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtka wa Serikali Seif Mohammed Khamis mbele ya hakimu wa mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji Muumin Ali Juma siku ya tarehe 25\03\2022 Majira ya saa 2 za Usiku huko Kinyasini Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, mtuhumiwa alimbaka msichana wa mwenye umri wa miaka 16 jina limehifadhiwa jambo ambalo ni Kosa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Kubaka kifungu cha 108(1)(2)(c) na 109(1) Sheria nambari 6\2018 Sheria ya Zanzibar.

Picha kutoka Maktaba.


Katika shitaka jengine, siku na tarehe isiyofahamika  Mwezi wa 04\2022 Majira ya saa 2 za Usiku huko Kinyasini Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba mtuhumiwa alimbaka msichana huyo.


Mshitakiwa baada ya kusomewa makosa yake alikana ndipo hakimu wa mahakama hiyo Muumin Ali Juma alipoamuru mshitakiwa kwenda Rumande Hadi tarehe 19\07\2022 Kasi yake itakaposikilizwa ushahidi.

Kesi hiyo yenye Nambari ya usajili 28\2022 kwa mara ya kwanza imesikiliza juzi July 05\2022 katika Mahakama ya Mkoa Chake Chake Pemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top