APELEKWA RUMANDE KWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MTU MWENYE ULEMAVU WA AKILI.

Hassan Msellem
0

 Na, Hassan Msellem, idawaonline.com Pemba.

Mahakama ya Mkoa Kusini Pemba Chake Chake amemrudisha Rumande Said Hassan Mabrouk almaarufu kwa jina la @SaidKing Mkaazi wa Mtoni Chake Chake kwa tuhuma za kumlawiti mlemavu wa akili mwenye umri wa miaka 35.

PICHA KUTOKA MAKTABA

Katika muendelezo wa kesi hiyo iliyosikilizwa June 28, 2022 mwendesha mashtaka wa Serikali Ali Amour Makame mbele ya hakimu wa mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji Muumin Ali Juma, imedaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa siku ya tarehe 10\05\2022 Majira ya saa 1:30 za asubuhi huko Mtoni Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mtuhumiwa alimlawiti mlemavu wa akili Jambo ambalo ni Kosa kisheria.

Shahidi nambari moja ambaye ni muathirika wa kesi hiyo ya udhalilishaji ameiambia mahakama kuwa siku ya tarahe 10\05\2022 majira ya saa 1:30 asubuhi mtuhumiwa alimchukuwa kutoka nyumbani kwao (muathirika) na kumpeleka nyumbani kwake (mtuhumiwa) na kumuingiza chumbani kisha kumvua nguo na kumlaza kifufdifudi na kumpaka mafuta sehemu yake ya siri ya haja kubwa na kumfanyia kitendo cha udhalilishaji.

“Alikuja kunichukua nyumbani na kunipeleka nyumbani kwake kisha akanitia chumbani na kunivua nguo akanilalaza kifudifudi akanipaka mafuta nyuma na kunifanyia kitendo hicho na alipomaliza akanambia nisiseme nyumbani”
alieleza muathirika huyo

Baaada ya ushahidi huo kutolewa ambao uliwaacha watu vinywa wazi hakimu Muumini Ali Juma alighairisha kesi hiyo hadi July 12, 2022 itakaposikilizwa tena ushahidi.

June 28, 2022 ni mara ya nne kesi hiyo kurindima mahakamani hapo, ambapo mara ya kwanza kesi hiyo kutajwa mahakamani ilikuwa ni May 23\2022, June 06\2022 na June 14\2022. 

TAZAMA VIDEO HII YA KUJITENGENEZEA PESA MTANDAONI UKIWA NYUMBANI.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top