ASKARI WA KIKE ACHENI UTEGEMEZI FANYENI KAZI.

0

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga SSP Debora Lukololo, amesema Askari wa kike Mkoani Mbeya wanatakiwa kufanya kazi Kwa bidii badala ya kuwategemea askari wa kiume kua kama nguzo Yao katika kazi.

PICHA KUTOKA MAKTABA


SSP Lukololo amesema hayo katika hafla maalum ya kuwaaga askari wa kike Mkoani Mbeya, walio staafu na wale walio hamishwa Mkoani humo kwenda katika Mikoa mingine, akiwemo SSP Debora Lukololo aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya wa Mbalizi na kuhamishiwa Mkoani Shinyanga.

Kwa upande wake askari mstaafu SGT Marry Yustino, aliye kua akihudumu katika dawati la jinsia Mkoani Mbeya amewaasa askari hao wakike kufanya kazi Kwa kufuata misingi na miongozo ya Jeshi la Polisi Ili kutoa huduma bora Kwa Wananchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top