ATUHUMIWA KUMUUA BINAMU YAKE WAKING'ANG'ANIANA KUCHAJI SIMU

0

 Polisi eneo la Kaimosi katika Kaunti ya Nandi wameanzisha msako wa kumnasa mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 17 kwa tuhuma za kumuua binamu yake anayetuhumiwa kwa mauaji ya binamu yake kwa kumpiga mshareKwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), mshukiwa alimuua Josephat Kibet mwenye umri wa miaka 31 kufuatia mzozo wa kung'ang'aniana sehemu ya kuchaji simu.

“Polisi eneo la Kaimosi, Kaunti ya Nandi wanamtafuta mshukiwa wa miaka 17 ambaye alimuua binamu yake jioni ya Jumapili kufuatia mzozo wa kuchaji simu,kufikia sasa uchunguzi unaonyesha kuwa wawili hao walikuwa wakizozana kuhusu ni nani wa kuchaji simu yake kwanza,” DCI ilisema kupitia kwa taarifa.

Mtuhumiwa inadaiwa alichomoa mshare na kumchoma nduguye kisha kutokomea kusiko julikana.


Josphat KIbet alikimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Kapsabet lakini alifariki hata kabla ya kufikishwa hospitalini.

“Josphat Kibet alithibitishwa kuaga dunia alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kapsabet kufuatia majeraha na mshale kutoka kwa kinda huyo,” taarifa ya DCI inasema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top