ATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA FIMBO KISA ELFU KUMI

0

Jeshi la polisi mkoani Manyara linamshikilia Petro Basso (38) mkazi wa Gabadaw wilayani Babati mkoani Manyara kwa kosa la kumpiga mkewe Maria Sakware (49) kwa fimbo na kumsababisha kifo huku chanzo kikielezwa kuwa mtuhumiwa kumtuhumu mkewe amechukua pesa yake kiasi cha shilingi elfu 10


Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Manyara

Kuzaga amesema kuwa kiini cha tukio hilo ni Ulevi wa mume wa marehemu na kumtuhumu marehemu kuwa amechukua pesa yake shilingi elfu 10 na kuanza kuchukua hatua mkononi kwa kumchapa na fimbo na kumsababishia majeraha mwili mwake ikiwemo maumivu katika mguu wake wa Kushoto pamoja na kumvunja mkono wa kushoto

Marehemu alifikishwa katika kituo cha Afya cha Bashnet kwa ajali ya kupata matibabu na ndipo umauti ulipomkuta

Hata hivyo Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kusababisha kifo cha mkewe na upelelezi utakapokamilika atafikishwa katika vyombo vya sheria.

TAZAMA VIDEO HII KAMANDA AKIZUNGUMZIA TUKIO HILO.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top