BWENI SHULE YA MSINGI LATEKETEA KWA MOTO CHALINZE

0

 BWENI la Shule ya Msingi ya wavulana ya Chalinze Modern Isalmic, iliyopo Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani limeungua moto na kusababisha uharibifu wa vifaa na hakuna madhara kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Bweni shule ya msingi lateketea kwa moto Chalinze

Akizungumza shuleni hapo alipotembelea shule hiyo iliyopo Chalinze Mzee kutoa pole na kujionea madhara ya moto huo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alisema tukio lilitokea alfajiri, wakati wanafunzi hao wakiwa kwenye ibada msikitini. 

Kunenge alisema hakuna wanafunzi walioumia na hakuna madhara ya kudhuru mwili na wataendelea na masomo kama kawaida na kuutaarifu umma kuwa, shule hiyo imepata changamoto ya tukio la moto, lakini wanamshukuru Mungu hakuna madhara yanayohusisha athari za kifya na maisha ya wanafunzi hao. 

"Vitu zikiwemo sare, mabegi, sabuni, na baadhi ya madaftari walivyokuwa wakikaa navyo kwenye bweni ndivyo vimeteketea kwa moto.

“Hakuna mwanafunzi atakaekosa masomo kwa sababu ya sare na shule hiyo ni kubwa, wanafunzi ambao bweni lao limeungua wamepata mahali pengine pa kulala na wataalamu tayari wameongea na vijana hao kuwatoa hofu na kuwashauri," alisema Kunenge.

Alilishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Pwani kwa elimu wanayotoa kwa shule za mkoa huo katika kudhibiti moto.

Naye Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani, Jenipher Shirima ameeleza kuwa moto huo umefanikiwa kudhibitiwa mapema kupitia vizimia moto vilivyopo shuleni hapo.

Mkurugenzi wa Chalinze Modern Islamic Primary School, Omary Ismail, alisema kuwa bweni lililoathirika ni la wavulana na vifaa vya wavulana nane ndiyo viliteketea vyote.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top