DK GWAJIMA ASEMA BIL 53/- KUKOPESHA WANAWAKE, VIJANA

0

 SERIKALI imetoa Sh bilioni 53.28 kwa ajili ya kukopesha wanawake, vijana na wenye mahitaji maalumu kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Bil 53/- kukopesha wanawake, vijana

Hayo yalielezwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima alipokuwa akihutubia akina mama katika maadhimisho ya siku ya batiki iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba. Alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh bilioni 62.6 zilizotengwa kwa ajili ya kuwainua kiuchumi wanawake, vijana na wenye uhitaji maalumu.

“Ili muweze kunufaika na fedha hizo, hamna budi kujiunga katika vikundi mbalimbali badala ya kuwa mmojammoja. Kwa mantiki hiyo, hamna budi kutengeneza batiki zenye ubora ambazo zinaweza kuuzwa nchini na kimataifa,” alisema.

Aliwapongeza akisema: “Kazi yenu ni nzuri, Rais (Samia Suluhu Hassan) anawathamini na serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika kuliletea taifa maendeleo.” Akijibu baadhi ya maombi ya Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Maendeleo, Rose Urio ya kutaka batiki kuwa vazi la taifa, Waziri Dorothy alisema atazungumza na viongozi wenzake lipate baraka kutoka kwa wadau mbalimbali serikalini.

“Maombi mengine ni kwamba serikali izungumze na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kiwekwe kipengele cha kujua ubora wa batiki ili kupunguza feki.” Kadhalika Rose alimuomba Dk Dorothy kama itawezekana wanawake wote wavae batiki Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8, kila mwaka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top