Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wamewatakiwa kuibua ajenda ambazo zitakuwa na maslahi kwa taifa ili kuwaongeza ushawishi katika Nyanja mbali mbali za maendeleo ikiwemo usawa wa kijinsia katika uongozi.
Akitoa mafunzo kwa waandishi wa
habari juu ya namna ya vyombo vya Habari na Utetezi katika ofisi za chama cha
waandishi wa habari wanawake Tanzania ‘TAMWA’ Mkanjuni Chake Chake Pemba katibu
wa klabu ya waandishi wa habari Pemba Ali Mbarouk Omar, alisema waandishi wengi
wamekuwa na tabia ya kuripoti matukio mbali mbali yanayotokeza katika jamii,
habari za mialiko ya kazi pamoja na ziara za viongozi na kuacha jukumu la
kuibua ajenda mbali mbali zenye maslahi ya umma jambo ambalo husabisha wananchi
kukosa haki zao.
Ameongeza kuwa kutokana na waandishi
wa habari kuliacha jukumu la kuiba ajenda badala yake jukumu hilo limekuwa
likitekelezwa na wanasiasa, viongozi wa Serikali pamoja wa watu maarufu, hivyo
basi amewaomba waandishi hao kulifanyia kazi suala la kuibua ajenda zenye
maslahi kwa umma ili kuongeza ushawishi katika mipango ya maendeleo.
“Jukumu la mwandishi wa habari ni
kuhakikisha anaibua ajenda zenye maslahi mapana kwa umma kupitia vyanzo mbali
mbali vya habari, lakini chakusikitisha ni kuona waandishi wengi wanakimbilia
kwenye kuripoti matukio mbali mbali yanayojitokeza katika jamii, kuandika
habari za mialiko pamoja na ziara za viongozi” alisema
Kwa upande wake, mratibu wa Tamwa Pemba
Fathiya Mussa Said, alisema miongoni mwa sababu zinazopelekea wanawake wengi
kushindwa kushiriki katika kugambania nafasi mbali mbali za uongozi ni pamoja
na majukumu ya kifamilia na ukosefu wa huduma bora za kijamii ikiwemo ukosefu
wa vitambulisho vya Uzanzibari mkaazi, Ukosefu wa maji safi na salama, huduma
za afya na nishati ya umeme.
Akiorodhesha baadhi ya maeneo ambayo
yanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa huduma vyeti vya kuzaliwa na
vitambulisho vya Uzanzibari mkaazi ni pamoja Makaazi, Kiungoni, Konde, Wingwi, Tumbe,
na Mtemani.
“Kwahivyo kuna changamoto nyingi sana
zinazowakabili akina mama kushindwa kujiingiza katika vyama vya siasa pamoja
kugombania nafasi mbali mbali za uongozi, ikiwemo ukosefu wa huduma bora za
kijamii, Vyeti vya kuzaliwa, Vittambulisho vya Uzanzibari Mkaazi pamoja
majukumu ya kifamilia, kwahivyo waandishi tunapaswa kuongeza nguvu ya utetezi katika
vyombo vyetu ili kuona changamoto hizo zinafanyiwa kazi” Bi. Fathiya Mussa Said
Aidha alisema, watetezi wa jamii wa
Wilaya ya Wete walifanikiwa kuibua changamoto ya ukosefu wa huduma ya kituo cha
afya huko Mjini Kiuyu na kugundua uwepo wa jengo la kituo cha afya ambalo
lilijengwa na wananchi na kuimba ofisi ya makamo wa kwanza wa pili wa rais Pemba
kusaidia millioni 34,064500 kwa ajili ya umaliziaji wa jengo hilo.
Mratibu wa Tamwa Pemba Fathiya Mussa Said akiwasilisha mada ya changamoto zinazowakabili wanawake katika kombania nafasi mbali mbali za uongozi pamoja kutokujishughulisha na shughuli za kisiasa.
Wakichangia mada katika mafunzo hayo,
baadhi ya waandishi wa habari wamesema ukosefu wa mazingira bora ya kufanyia
kazi, hali za kiuchumi pamoja na kutokuwa wabunifu ni miongoni mwa sababu
zinazochangia kutokufanya kazi zenye ubora na maslahi kwa umma.
“Ukiangalia unafanya kazi lakini huna
usafiri wala ofisi unayofanya kazi hakuna usafiri kwa ajili ya waandishi, huna
vifaa vyakufanyia kazi, huna nauli wengine ubunifu pia wakufanya hizo kazi
hawana tunawezaje kuibua ajenda na kuifanyia utetezi” alisema mmoja wa
waandishi hao
![]() |
Mwandishi wa kituo cha Radio jamii Micheweni na Jamii Tv Ali Massoud Kombo akichangia mada katika mafunzo hayo. |
Nao waandishi hao wameahidi
kubadilika, kuyatoa mafunzo hayo kwa waandishi wenzao pamoja na kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili yaweze kuleta tija kwa
taifa.
"kwakweli mafunzo ni mazuri sana yameongezea ujuzi wa kutosha, kwahivyo sasa waandishi ni jukumu letu kuyafikisha kwa waandishi wenzetu pamoja na kuyafanyia kazi napia tunaomba mafunzo haya yawe yanatolewa mara kwa mara ili tusiweze kuyasahau" Mchanga Haroub mwindishi wa ZBC.
![]() |
Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar 'ZBC' TV Mchanga Haroub kwa niaba ya waandishi wenzake akiahidi kuyafanyia kazi mafunzo hayo. |
KUHUSU MRADI
Mradi wa uhamasishaji wanawake
kushiriki nasafi za uongozi ‘SWIL’ una lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake
katika demokrasia ya uongozi katika ngazi za jamii na taifa kwa ujumla.
MALENGO YA MRADI
Ø Kuboresha uwezo wa wananchi 6000
ngazi ya jamii na taifa kuchukua hatua katika suala demokrasia na uongozi kwa
wanawake.
Ø Kushirikiana na wasanii 400 katika
uhamasishaji wa demokrasia kwa wanawake na haki ya kisiasa.
Ø Kuwawezesha waandishi wa habari 60
Unguja na Pemba kutoka vyombo tofauti kuandika habari za uchambuzi juu ya hali
ya demokrasia na wanawake na uongozi.
Ø Kuwezesha mfumo wa usimamizi na
tathmini katika kuwawezesha wanawake na uongozi pamoja na haki kisiasa.
WATEKEZAJI WA MRADI
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Tamwa, Zanzibar, Jumuiya ya Mazingira na Utetezi wa Kijinsia Pemba ‘PEGAO’ pamoja na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar ‘ZAFELA’.
WANUFAIKA WA MRADI
Wanawake, waandishi wa habari, jumuiya za kiraia pamoja pamoja na jumuiya ndogo ndogo zinazopatikana katika jamii.
WAFADHILI WA MRADI
Ubalozi wa Norway Tanzania.
MUDA WA MRADI
Miaka minne (4) kuanzia 2020 hadi
2023.