Waumini wa dini ya Kiislamu wameombwa kuzidisha maombi ili kuepushwa na janga la vitendo vya udhalilishaji linaloikabili Zanzibar.
kizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu katika mahafali ya Eid al-hajj yaliyoandaliwa na jumuiya ya Maimu Zanzibar(JUMAZA) huko Masjid Swabirinna Tundauwa Sheikh Zahor Saleh Omar ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo, amesema juhudi mbali mbali zimekuwa zikichukuliwa katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji lakini bado vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka, hivyo basi amewaomba waumini wa dini ya Kiislamu kuzidisha maombi ili kulitokomeza janga hilo.
Akisoma risala kaimu katibu wa jumuiya ya Maimu Zanzibar (JUMAZA) Sheikh Khamis Mwadini Khamis, amesema uwepo wa Klabu za Pombe nchini ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka Kwa matukio mbali mbali ya uhalifu ikiwemo vitendo vya udhalilishaji pamoja na wizi.
Aidha amesema jumuiya ya Maimu Zanzibar, inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo upungufu wa fedha.
Mahafali hayo ya Eid al-Hajj yaliyoandaliwa na jumuiya ya Maimu Zanzibar (JUMAZA) yamefanyika katika Masjid Swabirinna Utaani Tundauwa na kuhudhuriwa na waumini mbali mbali.
Baadhi ya akina Mama wa kiislamu walioshiriki kattika mahafali hayo.