Kijana mwenye umri wa miaka 19 Mkazi wa Wilaya ya Geita, William Bahelo amekutwa amefariki dunia kwa kujitia kitanzi ndani ya nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na Baba yake mkubwa iliyoko Mtaa wa Mbugani Mkoani Geita.
Akizungumza baada ya kufika kwenye eneo la tukio Shangazi wa William, Kabula Nairobi amesema hajui chanzo cha tukio la kufariki kwa Mwanae huku akiliomba Jeshi la Polisi kuchunguza kifo cha Mtoto wake.
RPC wa Geita Henry Mwaibambe amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo kwa njia ya simu huku akisema Jeshi linaendelea kuchunguza kifo cha kijana huyo ambacho kinahusishwa na ugomvi wa mali za Familia.
Aidha Kamanda Mwaibambe amezitaka Familia kuendelea kushirikiana katika kupunguza matukio haya ambayo yamekuwa yakiendelea juu ya ugomvi wa mali za Familia.