MBIO za Mwenge wa Uhuru leo umepokewa na kukimbizwa wilayani Bunda, katika Mkoa wa Mara alikozaliwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma ukitarajiwa kukagua miradi saba yenye thamani ya Sh. Mil. 985.778.
Pamoja na shughuli za makabidhiano kati ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Moses Kaegele na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassari, mradi wa kwanza kukaguliwa umekuwa wa madarasa tisa na ofisi tatu za walimu, katika Shule mpya ya Msingi Nyamuswa B. Geraruma alizaliwa katika Kata ya Nyamuswa, kijiji cha Bukama.
"Hivi mgekuwa mnaongoza mbio za Mwenge mngefanya maamuzi gani? Jengo lina nyufa ndani, nje zinashuka mpaka kwenye msingi wakati ujenzi haujakamilishwa," amesema Geraruma.
Ametangazia waliohudhuria tukio hilo kuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anawapenda, ndiyo maana anapeleka fedha za maendeleo kila kona ya nchi, lakini anaangushwa na wataalamu, watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia shughuli hizo.
Amekataa kuzindua mradi huo akisema hafuniki kombe mwanaharamu apite, kwani anatamani kuona nyumbani kwao kukiwa kuzuri, hususan sasa ambapo Rais Samia, anapeleka fedha kila kona ya nchi, kupeleka maendeleo kwa wananchi.
TADHALI USIPITWE NA HABARI HII TAFADHALI TAZAMA VIDEO HII