KORTINI KWA VIUATILIFU FEKI VYA MIKOROSHO

0

Kortini kwa viuatilifu feki vya mikorosho

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity Agro Industries inayodaiwa kusambaza viuatilifu feki aina Makonde Sulphur Dust  kwa ajili ya matumizi ya mikorosho, Haroun Maarifa amefikishwa Mahakama ya Mtwara akikabiliwa na mashtaka mawili.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Lugano Kasebele, mwendesha mashitaka wa serikali, Kauli George alieleza mahakama kuwa Mtuhumiwa anakabiliwa na mashtaka ya kukataa amri halali iliyoyolewa na mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa Viuatilifu (TPHPA) ya kuirejesha nchini Misri ilikozalishwa kiuatilifu aina ya Makonde Sulphur Dust 99%0 Batch No.3 yenye Usajili wa FU/0344 kilichothibitishwa kutokuwa na ubora.

Katika shtaka la pili, Mtuhumiwa anadaiwa kusambaza kiuatilifu hicho kisichokuwa na ubora kwenye vyama vikuu vya Ushirika vya MAMCU na TANECU kinyume na sheria.

Mwendesha mashitaka, George alidai mahakamani hapo kuwa kiuatilifu hicho kisicho na ubora kilisambazwa kwa chama Kikuu cha Ushirika MAMCU jumla ya Mifuko 2,480 yenye uzito wa kilo 25 kila kimoja  yenye thamani ya Sh 73,7800,000 na chama kikuu cha TANECU mifuko 1,251 yenye thamani ya Sh 37,217,250. Jumla ya thamani yote kuwa Sh 110,997,250.

Mtuhumiwa alikana mashtaka yanayomkabili na yupo nje kwa dhamana ya watu wawili na mmoja wao akiwa na mali zisizohamishika zenye thamani ya Sh milioni 50, huku mahakama ikiagiza mtuhumiwa kunyang’anywa hati yake ya kusafiria.

Kesi hiyo itatajwa tena Julai 28 mwaka huu kwa kuwa upelelezi unaendelea.

WANANCHI WANAOMBA ELIMU JUU YA SENSA TAZAMA VIDEO HII:


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top