LATRA-MARUFUKU MAHUBIRI NDANI YA MABASI,NI KINYUME NA KANUNI ZA USAFIRISHAJI

0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya mabasi kuruhusu biashara,Mahubiri mbalimbali ya dini na video zisizofaa kwa sababu ni kinyume na kanuni za usafirishajii.


Amepiga marufuku hiyo jijini Dodoma julai 26,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na kubainisha kuwa mamlaka hiyo ina jukumu kubwa la kudhibiti ubora ,viwango na usalama wa huduma.

Amesema kuwa biashara na kutoa mahubiri imeshakuwa tabia kwa baadhi ya vyombo vya Usafirishaji hapa nchini jambo ambalo limekuwa kero kwa wasafiri hivyo ni vyema wamiliki pamoja na watoa huduma kuachana kabisa na tabia hizo kwa sababu ni ukiukwaji wa kanuni zinazoongoza sekta hiyo.

"Kuanzia leo napiga marufuku biashara zote zinazofanyika kwenye vyombo vya usafiri na Mahubiri ni marufuku kufanya hivyo ni kinyume na sheria hivyo tabia hizo zikome ni kero kwa wasafiri" - Amesema Suluo.

TAZAMA VIDEO YA WAZIRI KINDAMBA AKITOA AGIZO LA WAKIUKAJI WA SHERIA.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top