Takribani Maduka 6 yameketea kwa moto ulioanza majira ya saa sita usiku katika eneo la National Housing Njombe mjini na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara.
Hadi sasa chanzo hakijafahamika huku mitazamo ikitofautiana kwa mashuhuda ambao baadhi wakisema kiini cha moto huo ni hitirafu ya umeme na wengine wakidai huenda mlipuko wa gesi ndiyo chanzo.
Kufuatia janga hilo kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Njombe imelazimika kufika eneo la tukio ikiongozwa na mkuu wa wilaya Kissa Gwakisa Kasongwa na kuvikunda vikosi vya jeshi la zimamoto vikiendelea na uokozi na kisha kutoa pole kwa wahanga wa janga hilo na hatua zinazokwenda kuchukuliwa na serikali.
Mbali na kukumbwa na janga hilo wakati wa uokozi wameibuka vibaka na kuiba mali zikiwemo simu jambo ambalo serikali imetoa onyo na kuahidi kuwasaka wahusika wote walioiba mali za wafanyabishara usiku wa manane.
Rotma Dauda ni ofisa operesheni kikosi cha zimamoto mkoa wa Njombe ambaye anasema wamefanya jitihada kubwa kuzima moto huo lakini changamoto kubwa ilikuwa kwa shirika la umeme ambalo nambari ya dharura zilikuwa haipokelewe ili kukata umeme huku mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara,Wenye viwanda na wakulima TCCIA mkoa wa Njombe Menard Mlyuka akisema wanasubiri tathimini ifanyike waone namna ya kuwashika mkono wahanga.
Mara baada ya kusikia kauli ya serikali na msimamo wa chama cha wafanyabiashara mkoani humo ,Kituo hikafanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara waliunguliwa maduka yao akiwemo Agnes Mangele ambao wanasema hadi sasa hawaelewi chanzo nini na kisha kuomba vyombo vya usalama kuchunguza na kuwatinguvuni vibaka walitumia mwanya huo kuiba mali wakati wa uokozi.
TAZAMA VIDEO YA AJALI YA MOTO KWA KUBOFYA VIDEO HII